The House of Favourite Newspapers

Wafahamu Mastaa Bongo Ambao Wamefanya Upasuaji wa Maumbo Yao

0

Urembo ni jambo muhimu sana na wanawake wengi hasa maarufu hufanya kila namna ili waweze kuwa na muonekano wanaoutaka, kuna wanaofanya upasuaji mkubwa wa viungo mbalimbali ili kuviweka katika maumbile wanayoyataka na wengine hufanya upasuaji mdogo kwa lengo la kupunguza mwili au uzito.

 

Hivyo basi katika makala hii nitakuletea wanawake maarufu wawili ambao wamefanya upasuaji na wanaonekana tofauti kabisa na awali.

 

MUNA LOVE
Mrembo wa kwanza ni Munalove kutoka nchini Tanzania, Muna Love alikua na muonekano mzuri sana ambao mwenyewe haukumvutia. Hivyo basi aliamua kubadilisha muonekano wake kwa kufanya upasuaji na kutaka aonekane kivingine kabisa yani awe Muna Love mpya.

 

Na mnamo mwezi November 2021 Kupitia ukurasa wake wa Instagram Muna Love alisema kuwa ” Naomba ndugu zangu na watu wangu wa karibu ambao wana picha zangu za zamani wazifute, kwani kwasasa nataka niwe naonekana nikiwa katika muonekano mpya yani kila kitu kwangu kitakua kipya na nishasahau kila kitu”.

 

Ikumbukwe ya kwamba Muna Love alifanya upasuaji wake nchini Uturuki, ambapo kila hatua aliyopitia alikuwa anashiriki na mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwaomba wamuombee. Ukizingatia upasuaji unaweza ukaleta madhara kwa mtu kama upasuaji huo utamkataa.

 

Tuangalie baadhi ya viungo alivyofanyia upasuaji Muna Love katika mwili wake,
1. Mashavu, ambapo alikuwa hana dimpozi lakini kwa sasa Muna Love ana dimpozi.
2. Shepu, kama tunavyojua Muna Love hakuwa mbaya lakini aliamua kufanya upasuaji na kuongeza shapu zaidi kuliko shape aliyokawa nayo awali.
3. Midomo ( Lipsi ), Munalove pia amefanya upasuaji wa Lipsi na kuwa na midomo mipya kabisa.

WEMA SEPETU
Kizamani zamani Wema Sepetu alijulikana kama Mrembo maarufu mwenye shepu nzuri na anavutia, lakini miaka michache iliyopita Wema Sepetu alifanya juhudi za kupunguza mwili na sasa anaonekana katika muonekano tofauti kabisa na zamani.

 

Wema Sepetu mambo yake hakuweka wazi wazi sana kama Muna Love lakini ilidaiwa kuwa mrembo huyo alifanya upasuaji na kupunguza utumbo ili awe anakula chakula kidogo, na kwa kufanya hivyo basi akawa amefanikiwa kupunguza mwili wake.

 

Tuhuma ya Wema Sepetu kupungua uzito ilikuwa gumzo sana kwa mwaka 2018 ambapo ilipelekea hadi madaktari kutoa kauli zao juu pasuaji mbalimbali zinazoendelea. Na wengi walisema kuwa upasuaji wa aina yoyote ule una madhara kwaiyo sio vizuri watu wakabana tumbo au kubadilisha muonekano wao walioumbiwa.

Leave A Reply