The House of Favourite Newspapers

WAFAHAMU VIUMBE WATATU WA KUTISHA WA BAHARINI

PAMOJA na kuwepo viumbe vikubwa na vya kutisha baharini leo hii, mnamo zama za kale palikuwa na viumbe wakubwa zaidi na wa kutisha zaidi kuliko wa leo na ambao wangeweza kuwameza papa na nyangumi tuwaonao leo baharini.  Wafuatao ni wanyama aina tatu wa kutisha waliokuwa wakiyatawala maji ya dunia mnamo zama za kale:

 

1. Shastasaurus
Shastasaurus ni mnyama mkubwa zaidi aliyepata kutokea baharini, akiwa na urefu wa mita 20 na alikuwa na umbile kama la pomboo (dolphin) na chakula chake kikiwa samaki.

2. Dakosaurus
Je, alikuwa samaki?  Alikuwa mmoja wa wanyama watambaao?  Au alikuwa na sifa zote mbili?Dakosaurus, aligunduliwa mara ya kwanza Ujerumani wakati wa muhula wa Jurassic, na alikuwa kiumbe  mwenye kula wanyama wengine.  Alifanana na mamba kidogo na alifikia urefu wa mita tano.

3. Megalodon
Ni jamii ya papa, mmoja wa viumbe wakubwa zaidi waliokuwa wakiwala wanyama wenzao.  Alikuwa ni mkubwa wa kutisha — mara tatu ya ukubwa wa papa tunayemfahamu leo. Aliweza kukua na kufikia urefu wa mita 20.

BABU TALE: “MAVOCKO Kufukuzwa WCB / DIAMOND Kuvaa KIKUKU”

Comments are closed.