The House of Favourite Newspapers

Wafahamu Wabunge Waliopita Bila Kupingwa

0

WAGOMBEA ubunge 28 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioingia katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi hizo walipita bila kupingwa baada ya kukosa wapinzani kutoka vyama vingine.  Hao ni wafuatao:

 

Job Ndugai kutoka Jimbo la Kongwa ambapo alikuwa spika wa Bunge la 11 la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, pia  alikuwa spika wa saba wa Bunge la Tanzania tangu uhuru.

 

Profesa Palamagamba Kabudi kutoka jimbo a Kilosa, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania katika serikali ya iliyopita. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

 

Dkt. Hamisi Kigwangalla alikuwa waziri katika serikali ya sasa na Mbunge wa Nzega Mjini.

 

January Makamba aliyekuwa Mbunge wa Bumbuli na aliyewahi kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais.

 

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa sasa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010.

 

HAWA NDIO WABUNGE 28 WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM , AMBAO WALIPITA BILA KUPINGWA

1. Job Ndugai (Kongwa)

2. Cosato Chumi (Mafinga Mjini)

3. Isaack Kamwele (Katavi).

4. Nape Nnauye (Mtama)

5. Kassim Majaliwab (Ruangwa)

6. Pauline Gekul (Babati)

7. Daniel Sillo (Babati Vijijini,)

8. Jummane Sagini (Butiama)

9. Ahmed Shabiby (Gairo,)

10. Prof Palamagamba Kabudi (Kilosa)

11. Godwin Kunambi (Mlimba)

12. Innocent Kalogeris (Morogoro Kusini)

13. Hamisi Taletale (Morogoro Kusini Mashariki)

14. Jonas Van Zeland (Mvomero)

15. Alexander Mnyeti (Misungwi)

16. Joseph Kamonga (Ludewa)

17. Enos Swale (Lupembe)

18. Ridhiwani Kikwete (Chalinze)

19. Kandege Sinkamba (Kalambo)

20. Joseph Mhagama (Madaba)

21. Iddi Kassim (Msalala)

22. Elias Kwandikwa (Ushetu)

23. Eng Godfrey Kasekenya (Ileje)

24. Philipo Mulugo (Songwe)

25. Rehema Migila (Ulyankulu)

26. Dkt. Hamisi Kigwangalla (Nzega Vijijini)

27. Januari Makamba (Bumbuli)

28. Jumaa Aweso (Pangani)

 

Leave A Reply