The House of Favourite Newspapers

WAFAHAMU WAIGIZAJI 5 WANAWAKE, WAKALI ZAIDI BARANI ASIA

WANAWAKE barani Asia wamekuwa na mvuto wa ajabu siku zote.  Hii ni kutokana na maelfu ya miaka ya kuendeleza utamaduni wao na urembo wao wa asili.  Miongoni mwao ni wanawake waigizaji watano wenye mvuto zaidi kutoka Bara la Asia.

10-stunning-asian-actresses-no-man-can-resist1a

Aishwarya Rai
Aishwarya Rai ambaye ni mwigizaji, hujulikana pia kama Indian Monica Belucci.  Ana mvuto wa aina yake na anafahamu lugha kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kitamil na Kibengali.  Mwaka 1994 alinyakua hadhi ya kuwa mwanamke mrembo zaidi duniani.

10-stunning-asian-actresses-no-man-can-resist2

Claudia Lynx
Hujulikana kama Mungu wa Kike wa Uajemi (Goddess of Persia).  Mwimbaji na mwigizaji huyu na mfasiri (wa lugha), ana mvuto wa aina yake unaomwongezea vionjo katika kazi za kusaidia jamii ambazo pia amekuwa akizifanya kwa muda mrefu.
10-stunning-asian-actresses-no-man-can-resist6

Priyanka Chopra
Miongoni mwa warembo ‘wakali’ wa India ni  Priyanka Chopra.  Yeye ana kila kitu kinachohusu urembo.  Ni mpenzi wa kazi za jamii pia, ambapo mwaka 2009 aliongoza filamu iliyoitwa Alert India kuhusu wagonjwa wa ukoma.  Mwaka uliofuata akawa balozi wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).10-stunning-asian-actresses-no-man-can-resist5a

Haifa Wehbe
Ni mwigizaji wa Lebanon anayejulikana sana Mashariki ya Kati kwani alianzia katika uanamitindo akingali binti mdogo na akatawazwa kuwa  ‘Miss South Lebanon’ alipokuwa na umri wa miaka 16 tu.10-stunning-asian-actresses-no-man-can-resist10a

Zhang Ziyi
Zhang Ziyi ni mwigizaji wa China aliyepata umaarufu katika filamu za ‘Geisha diaries’ na ‘The House of Flying Daggers’. Leo hii ni miongoni mwa waigizaji wanne wa China walio maarufu zaidi duniani.

Comments are closed.