The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara Kariakoo: Betika Linatupatia Mkwanja

0

MAPEMA leo Jumatano, Desemba 11, 2019, timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya wafanyabiashara wa Kariakoo na maeneo ya Kidongochekundu Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi za Gazeti la Betika.

Baadhi wa wafanyabiashara wa maeneo hayo wamelisifia gazeti hilo wakisema kuwa licha ya kutoa mwongozo wa kubeti lakini linawapa fursa ya kutangaza na gazeti hilo kwa viwango vya chini kabisa.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

Leave A Reply