The House of Favourite Newspapers

Waliozamia Sauz Wahukumiwa Kulipa Buku 50 – Video

0

WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akitoa msamaha kwa wafungwa wa makosa mbalimbali nchini Desemba 9, siku ya uhuru, wahamiaji haramu 19 raia wa Tanzania wamehukumiwa miezi miwili Gerezani na kulipa faini ya Shilingi Elfu Hamsini waliokuwa wamezamia kwenda nchini Afrika Kusini kinyume na sheria.

 

Hukumu hiyo, imesomwa leo Desemba 11 mwaka huu na Hakimu Mkazi, Victoria Mwaikambo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya washitakiwa hao kusomewa mashitaka yao na Mawakili wa Idara ya Uhamiaji Tanzania, Shija Sitta na Godfrey Ngwijo.

 

Washitakiwa hao wamesomewa maelezo ya makosa yao kisha wakakiri mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mwaikambo.

 

Mara baada ya kukiri makosa hayo, Hakimu Mwaikambo amewatia hatiani kwa makosa ya kutoka Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinyume cha Kanuni ya Uhamiaji pamoja na Kanuni ya 37 ya Kanuni za Uhamiaji G.N 657 ya mwaka 1997.

 

Baada ya kutiwa hatiani washitakiwa hao kwa nyakati tofauti walijitetea ambapo wengine walidai ni mara yao ya kwanza kutenda makosa ya namna hiyo, huku wengine wakiomba msamaha.

 

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mwaikambo amesema mahakama inawahukumu adhabu ya kifungo cha miezi 2 Gerezani sambamba na kulipa faini ya Shilingi Elfu Hamsini kwa kila mmoja.

 

Katika kesi hiyo namba 223 na 226 ya mwaka 2019 washitakiwa hao wanadaiwa kwa nyakati tofauti waliingia isivyo halali katika nchi ya Afrika Kusini bila kufuata taratibu za Idara ya Uhamiaji Tanzania.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave A Reply