The House of Favourite Newspapers

Wafanyabiashara wa Tanzania, Korea wakutana kujadili sekta ya ujenzi

Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Korea wakiwa katika picha ya pamoja. 
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Mada mbalimbali zikiendelea kutolewa katika mkutano huo.
Mkutano huo uliokutanisha  kampuni za Kitanzania na korea ukiendelea.
Mratibu wa kongamano hilo, Methew  Lubongeja (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki.

 

Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania na Korea, wamekutana na kujadili namna ya kukuza sekta ya ujenzi hapa nchini.

 

Mkutano huo umehusisha Kampuni ya Blue Mark ya Korea  na Jonta Investment ya Tanzania pamoja na baadhi ya Watanzania waishio nchini Korea ambao wamekutana na kujadili jinsi ya kukuza sekta ya ujenzi nchini Tanzania.

 

Akizungumzia kuhusu majadiliano hayo, mratibu wa kongamano hilo, Methew  Lubongeja amesema kuwa mazungumzo hayo hasa ni  kuwainua kiuchumi Watanzania katika sekta ya teknolojia kuelekea uchumi wa viwanda.

 

Alisema lengo la mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Sungwo, Korea ni kuunganisha wafanyabiashara wa Tanzania hasa wa sekta ya ujenzi na kampuni za Korea kuunganisha nguvu za pamoja.

 

Lubongeja aliongeza kwamba mkutano huo utaleta tija nchini Tanzania katika kuongeza nguvu za kufikia uchumi wa viwanda, ambayo ndiyo malengo ya Rais Dk. John Magufuli katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele.

NA DENIS MTIMA/GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.