The House of Favourite Newspapers

Wahamiaji Takribani 300 Wapotea Baharini wakitokea Senegal kuelekea Uhispania

0

Takriban watu 300 waliokuwa wakisafiri kwa boti tatu za wahamiaji kutoka Senegal kwenda visiwa vya Canary nchini Uhispania hawajulikani walipo, limesema shirika la misaada ya wahamiaji la Walking Borders siku ya jumapili.

 

Boti mbili, moja zikiwa zimebeba watu 65 na nyingine ikiwa na kati ya watu 50 na 60, zimepotea kwa siku 15 tangu walipoondoka Senegal wakijaribu kufika Uhispania, Helena Maleno wa Walking Borders ameliambia shirika la habari la Reuters. Boti ya tatu iliondoka Senegal Juni 27 ikiwa imebeba watu 200.

 

Familia za wale waliokuwemo ndani ya boti hizo hawajapata habari zozote kutoka kwa watu hao tangu walipoondoka, Maleno alisema. Boti zote tatu ziliondoka Kafountine kusini mwa Senegal, kiasi cha kilomita 1,700 sawa na maili 1,057 kutoka Tenerife, moja ya Visiwa vya Canary. Familia zina wasiwasi mkubwa.

 

Kuna takriban watu 300 kutoka eneo moja la Senegal. Watu hao wameondoka kwa sababu ya ukosefu wa utulivu nchini Senegal, Maleno alisema.

Leave A Reply