The House of Favourite Newspapers

Wajasiriamali Nchini Waanzisha Umoja wa HAYET kujikomboa Kiuchumi

0
Mkurugenzi Mkuu wa HAYET, Alhaj Noordin Kajuma akizungumza baada ya uzinduzi.

WAJASIRIAMALI nchini wameanzisha umoja wao walioupa jina la HAYET (Have You Eaten Today?) wakimaanisha umekula leo?

Lengo la umoja huo ni kuuziana bidhaa mbalimbali kwa bei ya kutupa.

Utepe ukikatwa kuashira uzinduzi huo, (kulia) ni Kaimu Shehe Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Sabbaha Makusi naye akishuhudia.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa umoja huo, Kinondoni Ada Estate jijini Dar, Mkurugenzi Mkuu wa HAYET, Alhaj Noordin Kajuma amesema umoja wao ndiyo utajiri wao.

Kajuma amesema wanachama wa umoja ambao umesajiliwa na serikali watauziana wenyewe kwa wenyewe bidhaa mbalimbali lakini lengo kuu ikiwa ni kuuziana chakula kwa bei nafuu ili kuikomesha njaa.

Askofu wa Kanisa la Dorcus Christian akiupongeza umoja huo wakati mkutano wa uzinduzi ukiendelea.

Wanaumoja huo wanatarajia kufanya maonesho ya bidhaa zao Oktoba 31 mpaka Novemba 8 mwaka huu makao makuu ya HAYET yaliyopo Kinondoni, Ada Estate karibu na Bar ya Four Ways ambapo wataanza kuuziana bidhaa hizo.

Meza kuu ikiwa makini kwenye uzinduzi huo.

Akisisitiza umuhimu wa umoja huo, Alhaj Kajuma alisema;

“Huyu akiwa na gari lake amelichoka anamuuzia kwa bei ya kutupa mwanaumoja mwenzake na yule friji lake kalichoka anafanya hivyo mwingine mazao, mifugo, viwanja na nyumba na kadhalika.

Sehemu ya wanaumoja wakisikiliza kinachoendelea.

“Nasisitiza kikubwa katika umoja wa HAYET ni kuuziana na kununua kwa bei za kutupa na ningependa mnada wetu unaotarajia kufanyika hapa Oktoba 31 mpaka Novemba 8 mwaka huu tuuite potelea mbali”. Alisisitiza Kajuma.      HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply