The House of Favourite Newspapers

Wajue nyota Samatta aliocheza nao Simba SC

0

Samatta-Waziri-Mkuu-15 Mbwana Samatta.

Na Said Ally
GUMZO hapa nchini ni juu ya mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta kutwaa tuzo ya mchezaji Bora wa Afrika kwa upande wa wachezaji waonacheza soka la ndani. Tuzo ambayo ni ya kwanza kwa hapa nchini.

Lakini mashabiki wengi wanamjua Samatta akiwa na kikosi hicho lakini hawatambui nyota ambao waliwahi kucheza na mshambuliaji huyo akiwa Simba. Makala haya yanakuchambulia nyota waliocheza nae akiwa ndani ya kikosi hicho na sasa wapo wapi.

kaseja

Juma Kaseja.

Makipa 
Juma Kaseja – Mbeya City
Mkongwe huyu alicheza na Samatta kwa kipindi kifupi mno ingawa kwa sasa amepungua umaarufu lakini bado yumo kwenye pilikapilika za soka, kwa sasa anaitumikia Mbeya City. Kwa inavyoonyesha, kawaida ya soka ilivyo, alipofikia Kaseja ni ndoto kutwaa tuzo kama ya Samatta.

Ally Mustapha ‘Barthez’ – Yanga
Kama ilivyo kwa Kaseja, baada ya kukaa Simba kwa muda, naye amesepa, yupo Yanga sasa ambapo amekuwa kipa wa kuaminika katika timu hiyo, naye kufikia mafanikio haya ya Samatta ni kazi ngumu kutokana na timu aliyepo.

Salum Kanoni – Kagera Sugar
Alikuwa anacheza beki ya kulia ambapo baada ya mambo kumuendea kombo akaihama Simba na kutua Kagera Sugar ambayo ndiyo anaitumikia mpaka sasa, anaingia katika mkumbo wa Kaseja na Barthez wa inavyoonyesha kufikia mafanikio ya Samatta ni ndoto.

Juma Jabu – Kagera Sugar
Alikuwa maarufu kama ‘JJ’ ambapo alifanya vyema akiitumikia nafasi ya beki wa kushoto ambapo naye baadaye alifungashiwa virago vyake na kujiunga Kagera Sugar. Ni ndoto kwake kuchukua tuzo hii

Nyosso1

Juma Nyosso.

Juma Nyosso – Mbeya City
Anatumikia kifungo cha miaka miwili ya kuwa nje ya soka kutokana na kumdhalilisha nahodha wa Azam, John Bocco. Kwake pia itakuwa ngumu kuona beki huyu siku moja akitwaa tuzo hii ya Samatta ingawa alikuwa moto enzi hizo.
Meshack Abel – Bandari

Aliwahi kwenda Kenya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Bandari lakini akarudi nchini msimu uliopita na kujiunga na Polisi Moro kabla ya mwaka huu kupotea na kusikujulikana .

Kelvin Yondani – Yanga
Beki kisiki anayeendelea kudunda akiwa na kikosi cha Yanga, licha ya uimara wake lakini itakuwa jambo la kusshangaza kuona ananyakua tuzo hii ya Samatta kwani umri nao siyo rafiki tena kwake.

Jerry Santo- Posta Rangers
Yupo kwao Kenya ambapo pia aliwahi kuichezea Coastal Union baada ya kuondoka Simba, hana matumaini yoyote kwa kuwa timu yake haiwezi pia kumbeba.

Abdulhalim Humud – Coastal Union
Bado anaendelea kucheza soka lake maridadi akiwa na Coastal Union ya Tanga ingawa aliwahi kuichezea timu ya Sofapaka baada ya kuondoka Simba. Kwa mambo yanavyoonyesha ndiyo ameshamaliza soka lake na kufikia mafanikio ya Samatta ni ‘Impossible’.

Mohamed Banka – Friends Rangers
Amebadili upepo sasa kwani yupo Friends Rangers ya daraja la kwanza baada ya kurejea akitokea Kenya alipokuwa na kikosi cha Bandari, alikuwa kiunga mahiri enzi hizo, maisha yamebadilika umri umemtupa mkono kufikia kwa Samatta.

Nico Nyagawa – Amestaafu
Aliwahi kuwa meneja katika klabu hiyo baada ya kuachana na soka ambapo sasa anashugulika na kikosi cha pili.

Hillary Echessa – Chemelil Sugar
Kama ilivyo kwa Santo, Echessa naye amerejea kwao na sasa anaitumikia timu ya Chemelil Sugar.

Amri Kiemba – Stand United
Yeye naye bado anakomaa kwenye soka ambapo yupo na kikosi cha Mfaransa, Patrick Liewig cha Stand United ya Shinyanga, hawezi tena kuwa bora na kufikia mafanikio haya.

Rashid Gumbo – Hajulikani
Aliwahi kwenda kucheza soka la kulipwa katika visiwa vya Shelisheli lakini kwa sasa hasikiki na haijulikani kama amepata timu ya kuichezea au la.

Patrick Ochan – URA
Ndiye aliyekwenda na Samatta katika klabu ya Mazembe lakini yeye hakuwa na nafasi sana ndani ya kikosi hicho na kujikuta akitimkia katika klabu ya URA ya Uganda, naye kwa hali inavyoonyesha kufikia mafanikio ya Samatta ni ngumu na haitawezekana.
Emmanuel Okwi – Sonderjyske
Kipenzi cha mashabiki wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Sonderjyske ya Denmark, Mganda huyu labda akirudi Afrika kuna siku anaweza kutwaa tuzo hii.

Mussa Mgosi – Simba
Ndiye nahodha wa Simba kwa sasa lakini amekuwa akikosa nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha kwanza ingawa alikuwa bora sana wakati Samatta anacheza, kufikia levo za Samatta kwa kipindi hiki ni ngumu kwake.

Ahmed Shiboli – Coastal Union
Amejiunga katika kikosi hicho msimu huu baada ya kutamba na African Sports alipokuwa nayo daraja la kwanza, haitawezekana tena kufikia kwa Samatta.
Amir Maftah – Friends Rangers
Yupo daraja la kwanza na timu ya Friends Rangers, taswira ya kuchukua tuzo imefifia mno.

Uhuru Suleiman – Royal Eagle
Anacheza soka la kulipwa katika timu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini lakini ametolewa kwa mkopo kwenye timu ya Royal Eagles, labda kwa maajabu ya Mungu lakini kwa sasa ni ndoto kufikia kwa Samatta.

Joseph Owino – Uganda
Alitimka ndani ya kikosi hicho na kurejea kwao katika timu ya Tusker. Hana misimu mingi sana ya kucheza soka, hivyo kufikia kwa Samatta ni ndoto.

Leave A Reply