The House of Favourite Newspapers

Wajumbe Wamwidhinisha Biden Rais, Bye-Bye Trump!

0

JOPO la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, maarufu kama Electoral College limemthibitisha Joe Biden kuwa rais ajaye wa wa taifa hilo.

 

Hatua hiyo inatajwa kuifunga milango kwa mpinzani wake, Donald Trump, katika jitihada zake za kisheria za kuyageuza matokeo ya uchaguzi wa 2020.

 

Hatua hiyo inafanyika huku mteule huyo akimkosoa mpinzani wake huyo kwa maneno makali tangu kumalizika kwa uchaguzi kwa kumwita mpinga matakwa ya umma na mkaidi katiba ya nchi.

 

Wajumbe wakiwa wamepiga kura siku ya Jumatatu, walimpa rasmi Joe Biden zaidi ya kura 270 za uchaguzi zinazohitajika kuthibitisha ushindi wake wa uchaguzi.

 

Pamoja na kura 55 za wajumbe kutoka California, kati ya za mwisho kupigwa Jumatatu, Biden ana kura 302 za uchaguzi, zaidi ya kiwango kinachohitajika kushinda urais.

 

Biden amekuwapo kwenye uwanja wa siasa za Marekani kwa karibu nusu karne, na ushindi wake katika kura za wajumbe umemfanya Trump, Mrepublican, rais wa tano wa Marekani katika historia ya miaka 244 ya nchi hii kupoteza uchaguzi baada ya muhula mmoja katika Ikulu ya Marekani.

 

Kura ya wajumbe ni ya uthibitisho wa utaratibu wa kawaida kwenye kalenda ya uchaguzi wa urais wa Marekani.

 

Lakini tangu kura ya kitaifa ya Novemba 3,  2020, Trump amedai mara kwa mara bila ushahidi wwowote wa kuaminika kwamba kura katika majimbo yaliyokuwa na ushindani mkali aliyopoteza kwa Biden kwa viwango tofauti ilikuwa ya wizi ikimgharimu kuchaguliwa tena.

 

Trump na washirika wake wamepoteza kesi zaidi ya 50 katika majimbo yenye ushindani mkali wanakopinga matokeo ya kura hiyo.

Leave A Reply