The House of Favourite Newspapers

Wakali 40, Jukwaa Moja Singeli ‘Kuwaka Moto’ Nyerere Day Dar Live Leo

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HAIJAWAHI kutokea! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine pale wakali wa muziki ulioshika kasi kama kiberenge ‘Singeli’ zaidi ya 40 watakapopanda jukwaa moja la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Unajua kitatokea nini? ‘Moto utawaka.’

Waambie na wenzio! Shoo ya kihistoria, ya kibabe na ya Kiswazi inatarajiwa kuweka historia kwa mara ya kwanza ukumbini hapo, leo Ijumaa ya Oktoba 14, mwaka huu ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius Nyerere ‘Nyerere Day’.

sholo-mwamba-1021x580

Sholo Mwamba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo, alisema kuwa, shoo hiyo itatambulika kwa jina la Singeli Michano ambapo wakali wa muziki wa Singeli zaidi ya 40 watakinukisha jukwaa moja.

“Itakuwa ni zaidi ya historia kwani haijawahi kutokea nchini wakali wa muziki wa aina moja kupafomu jukwaa moja tena, kwa wakati mmoja, hii ndiyo mara ya kwanza.

step0002
“Unajua tangu muziki huu wa Singeli uanze, hatujawahi kuona wanamuziki hawa wakipafomu jukwaa moja ndiyo maana sisi kama Dar Live tumeamua kuwaleta pamoja ili wale wapenzi wa muziki huu wanaousikia tu wapate ladha za tofauti kwa kushuhudia kwa macho yao,” alisema Mbizo.

Mbizo aliongeza kuwa, mara zote Dar Live imekuwa ikileta vitu vya tofauti ambavyo ni adimu kuvipata katika ukumbi wowote nchini, hivyo katika shoo hii ya Singeli Michano mashabiki watarajie kupata vitu hivyo adimu.

“Tunatarajia hapo baadaye kuwa na orodha ndefu ya wakali zaidi ya 40 watakaopafomu kwenye jukwaa moja lakini hadi sasa ambao tutakuwa nao ni Dogo Niga, Majid Migoma, Dula Makabila, Msaga Sumu, Kaju Mpamba, Sholo Mwamba na Segere.”

Pamoja na kutaja majina ya baadhi ya wanamuziki watakaopafomu jukwaa moja na kuimba muziki huo wa aina moja, Mbizo pia alisema shoo hiyo itaanza rasmi mida ya saa 8:00 mchana na kuendelea mpaka usiku mnene huku kiingilio kikiwa kiduchu cha shilingi 5,000 tu kwa kila atakayeingia ukumbini hapo.
“Tunaposema haijawahi kutokea tunamaanisha, shoo nzima wakali zaidi ya 40 jukwaa moja kiingilio 5,000 tu uliona wapi kama siyo Dar Live pekee?

“Kikubwa niwaombe tu wapenzi wa burudani hasa wa muziki wa Singeli kuja kwa wingi ili kuburudika na kuona nani mkali zaidi kwenye muziki huo ambao umeteka soko la muziki kwa sasa na unapendwa na watu wa rika zote, wakiwemo watoto, vijana mpaka wazee,” alisema Mbizo.

Comments are closed.