The House of Favourite Newspapers

Wakali wa Mitindo Afrika… Wapo Hapa

Mrembo kutoka Bongo ambaye alishinda Shindano la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana Matata.

MIONGONI mwa tasnia kubwa duniani, katika masuala ya burudani ukiachana na muziki na filamu, tasnia nyingine ambayo ina mashabiki wengi ni ya mitindo. Wafuatao ni warembo kutoka Afrika ambao wameleta ushindani mkubwa kwenye soko la mitindo duniani:

FLAVIANA MATATA

Mrembo kutoka Bongo ambaye alishinda Shindano la Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na kuliwakilisha taifa kwenye Shindano la Miss World Universe, alipofanikiwa kushika namba sita. Flaviana anaingia kwenye listi hii kutokana na mchango mkubwa aliouweka kwenye ulimwengu wa mitindo. Amekaa kwenye makava mengi ya magazine ikiwemo, Dazed & Confused, Glass Magazine na L’Official.

 

Mwaka 2011, Flaviana alishinda Shindano la Mwanamitindo Bora wa Mwaka lililoandaliwa na Jarida la Arise la nchini Nigeria, na kwa sasa ana mkataba na kampuni iitwayo Wilhelmina Modelling Agency ya jijini New York, Marekani.

 

FATIMA SIAD

Mwanadada huyu ni raia wa Somalia mwenye asili ya Ethiopia. Fatima ana mkataba na Kampuni ya IMG Models New York City, Paris, Milan na London, pamoja na Kampuni ya Ace Models ya Athens, Ugiriki. Lakini pia ana mkataba na Kampuni ya Munich Models ya Ujerumani na pia amewahi kutokea kwenye magazeti ya Essence Magazine, Look Magazine UK, Avon’s Mark Catalog, Ebony Magazine na Marie Claire.

 

LIYA KEBEDE

Mwanadada huyu kutoka Ethiopia ni miongoni mwa warembo waliofanikiwa kwenye ulimwengu wa mitindo Afrika lakini pia ni muigizaji ambaye ameshiriki kwenye muvi za The Best Offer (2013), Lord of War (2005) na Desert Flower (2009). Liya ndiye
mwanamitindo wa kike wa kwanza wa Kiafrika kupamba jarida la Vogue kwa miaka mitano mfululizo, yaliyochapishwa kwenye nchi za Italia, Japan, Marekani, Ufaransa, Hispania na kwenye majarida ya V, Flair, i-D na Time’s Style & Design.

 

MARIA BORGES

Mrembo huyu kutoka Angola naye ni namba nyingine kwenye ulimwengu wa mitindo. Amefanya matangazo mengi pamoja na kuuza sura kwenye majarida mbalimbali yakiwemo Ralph Lauren, Versace, Tom Ford, Emporio Armani, Victoria’s Secret, Giorgio Armani na matangazo ya makampuni na brand za C&A, Givenchy, H&M, Oscar de la Renta na Tommy Hilfiger.

 

ALEK WEK

Mwanadada Alek, ni mwanamitindo kutoka Sudani ambaye alianza mambo ya mitindo akiwa na umri wa miaka 18, mzaliwa wa Sudani Kusini lakini amekulia jijini London, Uingereza. Alek ameshiriki kutangaza brand na majarida ya Issey Miyake, Moschino, Victoria’s Secret, Clinique, Shiatzy Chen, John Galliano, Chanel, Donna Karan, Calvin Klein, Jasper Conran, xander McQueen, Givenchy, Armani, Fendi na Christian Dior.
Makala

Comments are closed.