The House of Favourite Newspapers

Mauzo ya Soko la Hisa Yashuka

1

 

Ofisa Mwandamizi Masoko, Soko la Hisa, Mary Kinabo, akizungumza na wanahabari.

 

Mauzo ya Hisa (Turnover/Liquidity) Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa milioni 2.39 wiki iliyoisha tarehe 23 Juni 2017, hadi hisa 335,000 kwa wiki iliyoishia June 30, 2017.

Hivyo pia thamani ya mauzo ya hisa kupungua kutoka Shilingi bilion 19 wiki iliyopita hadi Shilingi milioni 412 wiki hii iliyoishia tarehe 30 Juni 2017.

Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:

TCC …………………………………………..……70.41%

CRDB ……..…….………………..…………..………11.86%

TBL ………..……..……….…………….………… 7.97%

Ukubwa wa Mtaji (Market Capitalization)

Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepanda kwa Shilingi Bilioni 438 kutoka Shilingi Trilioni 18.8 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.2 wiki iliyoishia tarehe 30 Juni 2017.

 

 

Hii ni kutokana na kupanda kwa bei za hisa za USL (15.38%), TCC (12.76%) na KA (7.14%). Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 124 kutoka Shilingi Trilioni 7.6 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.75 wiki hii.

 

Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za TCC (12.76%). Hati Fungani (Bonds) Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 30 Juni 2017 yamepanda kutoka Shilingi milioni 770 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 9.6 mauzo haya yalitokana na hatifungani nne (4) za serikali na za Makampuni zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 11.04 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 9.6.

 

Viashiria (Indices) Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 40 kutoka pointi 2,127 hadi pointi 2,166 kutokana na kuongezeka kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.

 

Kufuatia kupanda kwa bei za hisa, kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 59 kutoka pointi 3,632 wiki iliyopita hadi pointi 3692 wiki hii. Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) imepanda kwa pointi 110 kutoka pointi 4,803 wiki iliyopita hadi pointi 4914 wiki hii kutokana kupanda kwa bei za hisa za TCC kwa 12.76% kutoka Shillingi 9800 hadi 11,050.

 

 

Kiasharia cha huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii kimepungua kwa pointi 0.6 kutoka pointi 2,515 hadi pointi 2,514.64 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za DSE (1.69%) Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa 2,467 kama awali.

 

Shindano la Wanafunzi la Uwekezaji Shindano la DSE SCHOLAR INVESTMENT CHALLENGE 2017 lilifika mwisho tarehe 30 Juni 2017. Zaidi ya wanafunzi wa vyuo na secondary 11,000 walishiriki katika shindano la mwaka huu, ikiwa ni Zaidi ya mara 3 ya mwaka uliopita, 2016.

Matokea ya washindi wa shindano hili yatatangazwa tarehe 10 July zoezi la uchambuzi litakapoanza.

 

Matokeo ya washindi wa Soko la Hisa (DSE) Kutangazwa Julai 10, zaidi ya wanafunzi 11,ooo wa Sekondari na vyuo walishiriki

Imetolewa na Mary Kinabo, Ofisa Mwandamizi Masoko, Soko la Hisa.

1 Comment
  1. […] uwekezaji wa hisa lililojumuisha wanafunzi wa shule na vyuo mbalimbali lililokuwa likiendeshwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam, Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) limefikia tamati, ambapo washindi wamepatikana […]

Leave A Reply