The House of Favourite Newspapers

SHINDANO LA MAMILIONI KWA WANAFUNZI LAIBUA WASHINDI

0
Benson Mcharo akiwa ameshikilia mfano wa hundi ya fedha ya ushindi wake.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa, Bw. Molemi Marwa akimpongeza Benson kwa ushindi wake.
Bw. Mawa akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Tanzania (NEEC), Beng’i Issa akizungumza katika hafla hiyo.
Marry Kinabo wa Soko la Hisa akizungumza jambo.
Hafla ikiendelea.

HATIMAYE lile shindano la uwekezaji wa hisa lililojumuisha wanafunzi wa shule na vyuo mbalimbali lililokuwa likiendeshwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam, Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) limefikia tamati, ambapo washindi wamepatikana na kutangazwa wazi majina yao na kujinyakulia kitita cha pesa kutokana na nafasi za ushindi wao.

Kwa upande wa wanafunzi wa vyuo, mshindi wa kwanza alitoka  Chuo Kikuu cha Kilimo na Ufugaji cha Sokoine (SUA), akitajwa kwa jina la Benson Mcharo ambaye amejinyakulia zawadi ya Sh. Milioni 2.

Irene David, yeye ameongoza kwa wanafunzi wa shule za sekondari, ambapo amejinyakulia kitita cha shilingi milioni 1, akitokea shule ya Scolastica ya wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Katika hafla hiyo aliyekuwa mgeni rasmi ya ugawaji tuzo hizo alikuwa ni  Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Tanzania (NEEC), Beng’i Issa ambaye wakati akizungumza aliipongeza DSE kwa kuandaa shindano hilo kwa kuwa linasaidia kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji kwa wanafunzi nchini.

Nao washindi hao, kwa nyakati tofauti walitoa shukrani zao kwa DSE huku wakieleza nia na malengo ya ushiriki wao kwenye kinyang’anyiro hicho.

Leave A Reply