The House of Favourite Newspapers

Wakazi Bonde La Mto Msimbazi Leo Ikiwa Siku Ya Mwisho Kuishi Eneo Hilo Baadhi Hawana Pakwenda

0
Bi Zainabu Madenge ambaye nyumba yake ilikuwa na vyumba vitano pesa aliyopewa imetosha kujenga vyumba viwili tu maeneo ya Chanika Dar.

Dar es Salaam 12 Aprili 2024: Waliokuwa wakazi wa Bonde la Mto Msimbazi ambao wametakiwa kuhama maeneo hayo baada ya kulipwa fidia ya makazi waliyokuwa wakiishi baadhi yao wamesema hawana pakwenda kufuatia pesa waliyolipwa kushindwa kutosheleza kununua viwanja na kumudu gharama za ujenzi.

Waandishi wetu leo hii walitembelea maeneo hayo na kuzungumza na wakazi hao ambao wengine walikuwa wakiendelea kubomoa nyumba zao kwa hiyari na wengine kuhamisha vitu vyao.

Miongoni mwa wakazi hao ni bibi mjane Suzana Evarist na bibi Zainab Madenge ambao wamekutwa waeneo hayo.

Bibi Mjane Suzana Evarist akiwa hajui lakufanya ambapo amesema mafao aliyopewa hayamtoshi kununua kiwanja na kujenga nyumba kama aliyokuwa akiishi.  HABARI/PICHA RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL
Leave A Reply