The House of Favourite Newspapers

Wakazi wa Dar Wanufaika na Promosheni ya Tusua Ada na Omo

Meneja wa Game Supermakert ya Mlimani City, Josephat Okumu (kushoto), akimkabidhi mshindi wa droo ya pili, Grace Mboka mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea.Dro hiyo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket hiyo.Katikati ni Meneja wa Omo, Upendo Mkusa.

WAKAZI sita wa jiji la Dar es Salaam wafanyao manunuzi katika Supermarket za Game, Choppies Mlimani City na Shoppers Mikochen, Masaki na Mbezi wamejishindia jumla ya shilingi milioni tatu(3,000000) ikiwa ni shilingi laki tano (500,000/=) kila mmoja baada ya droo ya pili kufanyika mwishoni mwa wiki.

Washindi hao walipatikana mara baada ya kununua Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa inayochezeshwa katika Supermakert kila jumamosi.

Meneja msaidizi wa Coppies Supermaket ya Mlimani City Edger Matilya(kulia), akimkabidhi mshindi wa droo ya pili, Shidu Abubakari mkazi wa Tegeta Dawasco jijini Dar es Salaam pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada na Omo” inayoendelea.Dro hiyo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket hiyo.Katikati ni Meneja wa Omo, Upendo Mkusa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Meneja wa Omo, Upendo Mkusa kwanza aliwapongeza washindi wote haswa watatu waliopatikana katika droo ya pili kukamilisha idadi ya washindi sita ambao ni Grace Mboka mkazi wa Goba aliyeshinda katika Supermaket ya Game Mlimani City, Shidu Abubakari alishinda katika Supermaket ya Choppies Mlimani City na Lilian Patrick aliyeshinda katika Supermakert ya Shoppers ambapo aliwaomba pesa walizoshinda wakazielekeze kwenye elimu kwa watoto wao kama kauli mbio ya kampeni inavyo sema “Tusua Ada na Omo”.

Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Sabuni ya Omo wanatambua kama jamii ya Watanzania imetoka katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya hivyo wakaona ni jambo jema kuungana na wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto kwenda shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupitia promosheni hii.

Comments are closed.