The House of Favourite Newspapers

Wakazi Wa Mji Wa Moshi Kuinjoi Wifi Ya Tigo Bure Kipindi Cha Mbio Za Tigo Kili International Half Marathon

0
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini ndugu Henry Kinabo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari leo.

Kilimanjaro 20 Februari 2024: Kampuni ya mawasiliano ya Tigo imetangaza kuja na mtandao wa 5G mkoani Kilimnajaro wakati huu wa Msimu  wa Mbio za kimataifa za  Kilimanjaro Marathoni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini ndugu Henry Kinabo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari moshi mjini mkoani Kilimanajaro leo, February 20  kuelekea katika mbio za Kilimanjaro marathon zinazotarajia kufanyika February 25 mwaka huu.

Kinabo amesema kampuni hiyo ya Tigo ambayo ni wadhimini wa mbio hizo kwa mwaka wa tisa mfululizo imejizatiti kuendelea kuwa bora katika utoaji wa huduma za mawasiliano na hii ni kutokana uwekezaji mkubwa ambao wameufanya katika seka hiyo.

Ameongeza kuwa katika kipindi chote cha mbio hizo  mwaka kuu  Tigo itatoa huduma ya wifi bure katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi sambamba na ofa kadhaa kwa wakimbiaji na wateja wao hivyo kila mmoja anapaswa kuchangamkia fursa hiyo.

Aidha baada ya kumalizika kwa mbio hizo za  Kilimanjaro Marathon  kampuni hiyo ya mawasiliano inatarajia kuzindua mradi wa uoteshaji miti uitwao Tigo Green For Kili wenye lengo la kuotesha miti ipatayo elfu thelathini kama sehemu ya kuchagiza uhifadhi wa mazingira.

Kampuni ya Tigo  ni wadhamini  wa mbio za kimataifa za Kiliamnajaro  marathon hususani zile za kilomieta 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon.

Leave A Reply