The House of Favourite Newspapers

Wakili Jerome Msemwa Ajitoa Rasmi Kumtetea Malinzi na Wenzake

0

Wakili Jerome Msemwa leo ametangaza kujitoa katika kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho la Mpira nchini(TFF), Jamal Malinzi na Wenzie wawili(Celestine Mwesigwa na Nsia.

Msemwa ambaye alikuwa akiwatetea washtakiwa hao, ameandikia barua kwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri leo July 5, 2017 akieleza amejitoa katika kesi hiyo kutokana na kutopata maelekezo sahihi kutoka kwa wateja wake.

Viongozi hao wanakabiliwa na mashtaka 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na ufisadi.

Soma walaka wake huu

Leave A Reply