The House of Favourite Newspapers

Wakongwe wa muziki walivyoiteka Dar Live, Valentine’s Day

0

2Mkongwe Ali Star akifanya yake na bendi ya TOT.
3Abdul Misambano akikamua.
4Khadija Kopa akifanya ‘mavituz’ yake.1Waimbaji wa TOT wakitumbuiza moja ya nyimbo zao.
10Mkongwe Hassan Bitchuka akiimba kwa hisia.
8Roman Mng’ande akikamua sambamba na Msondo Ngoma.
12Mkongwe Shaban Dede akiwakumbusha vijana wa zamani moja kati ya vibao vyake.
11TX Junior akiimba moja ya vibao vya Msondo.9Shabiki aliyeshindwa kujizuia hisia zake akijimwaga.

za muziki wa dansi za Sikinde, Msondo na African Stars ‘Twanga Pepeta’ zikisindikizwa na bendi ya muziki wa Taarabu, Tanzania One Theatre ‘TOT’, jana waliweka historia ya kutoa burudani mfululizo Siku ya Wapendanao waliofurika katika ukumbi wa maraha wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Shoo hiyo ilianza kwa bendi ya TOT kutoa burudani ikiongozwa na Khadija Kopa kisha wakafuatia Sikinde wakiongozwa na mkongwe Hassan Bitchuka.

Baada ya Sikinde kushuka walipanda Twanga Pepeta wakiongozwa na Ali Chocky kabla ya wao pia kupokelewa na ‘Baba ya Muziki’, Msondo Ngoma, wakiwa na wakongwe kibao kama vile Shaban Dede, Saidi Mabera, Romario na wengine kibao.

Burudani hiyo iliyodhaminiwa na Global Publishers, Johannesburg Hotel na Dar Live ilienda kwa mtindo wa bandika-bandua kwa bendi zote kupiga kwa kupokezana kabla ya kuhitimishwa kwa disko kali kutoka kwa DJ Max aliyekinukisha hadi majogoo.

(Picha: Chande Abdallah, Issa Mnally na Gabriel Ng’osha/ GPL)

Leave A Reply