The House of Favourite Newspapers

Wakulima Wadogo Kunufaika na Mikopo Kutoka Benki ya Maendeleo

1

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Francis Assenga (kulia) akizungumza na wanahabari. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Albert Ngusam.

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank-TADB) imesema kuwa wakulima wadogo wataanza kunufaika na mikopo kutoka katika benki hiyo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADP, Francis Assenga, amesema kuwa wakulima wadogo angalau watawezeshwa kupatiwa mikopo ya shilingi laki tano ikiwa ni mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo kutoka benki hiyo.

Alisema benki hiyo ilianzishwa ikiwa na malengo ya kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

2

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha Mei hadi Desemba mwaka jana, 2016, kuwa ilikopesha kutoka kiasi cha kuanzia shilingi bilioni moja hadi shilingi bilioni 6.5 kwenye vikundi kuanzia nane hadi kufikia 20, kutoka wakulima 944 hadi kufikia 2572.

NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.