The House of Favourite Newspapers

Wakurugenzi Watakaokusanya Chini ya 50% Kuondolewa

0

Waziri Jafo

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri 185 Nchini kuhakikisha wanafikisha zaidi ya 50% ya makusanyo ya mapato ifikapo Januari 15, 2021.

 

Amesema Januari 15 atatatoa taarifa ya miezi 6 ya ukusanyaji mapato, hivyo Wakurugenzi wote 185 wakajipime maana hataki kuona Halmashauri iliyopata chini ya 50%.

 

Makusanyo yataonesha kama Mkurugenzi anafaa kuendelea na Serikali ya awamu ya tano au awekwe pembeni aje mwingine anayeweza kukusanya mapato.

 

Aidha, hawatashughulika Wakurugenzi peke yake bali pia Watunza Hazina pamoja na Maafisa mipango, hili ni agizo langu kwa Halmashauri zote Nchi nzima.

Leave A Reply