The House of Favourite Newspapers

Walezi wa Wana Wajengewe Sanamu

0

MUZIKI wa Bongo Fleva unatajwa kuongoza kwa kuwa na mashabiki wengi kwa sasa nchini. Kupitia fani hii, vijana wengi wamejiajiri na kuendesha maisha yao.

Ukiachana na watoto wa kiume ambao wengi wao wanaonekana kuukubali muziki huo, pia wapo watoto wa kike hasa mastaa wa Bongo Muvi ambao ndiyo unaweza kusema wanauelewa kinoma.

 

Ndio! Hilo halina ubishi. Mfano mzuri ni hivi sasa msanii wa Bongo Fleva akiachia ngoma, basi utaona warembo wa Bongo Muvi kama wote wakijirekodi wanaimba, lakini pia amekuwa wakishirikiana nao hata katika matamasha ambayo wanayaandaa.

 

Warembo hao miaka ya nyuma walikwenda mbali zaidi na kutoa sapoti kwa wasanii wa Bongo Fleva na kuwafanya hadi leo hii wajulikane zaidi na kazi zao zikubalike.

 

IJUMAA linakuletea listi ya baadhi ya mastaa wa Bongo Muvi ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye Bongo Fleva ambao wamepewa jina la walezi wa wana wanaopaswa kujengewa sananu;

 

WEMA

Mwanadada mrembo aliyejinyakulia Taji la Miss Tanzania 2006, Wema Issac Sepetu aliingia kwenye mahaba mazito na Mtoto wa Tandale, Nasibu Abdul ‘Diamond; enzi hizo Chibu wa watu akiwa ndiyo anajitafuta kwenye Bongo Fleva.

 

Licha ya kwamba alisemwa mno kipindi hicho kuwa kwa nini anatoka na mwanaume ambaye haendani naye, lakini wala TZ Sweetheart hakulijali hilo kwani aliendelea kumsapoti hadi walipokuja kutengana mazima na staa huyo kuhamishaia majeshi kwa mwanamama wa mwenye asili ya Kiganda, Zari The Boss Lady.

 

Itoshe kusema kwa sasa Diamond ndiye staa mkubwa Tanzania ambaye kwa bidii zake na sapoti ya Wema amefanikiwa kuitangaza Bongo katika mataifa mbalimbali hivyo unapomsifia Diamond au Mondi usisahau kumsifia na Wema pia ambaye utamuona kwa uzuri kwenye ile Video ya Moyo Wangu.

 

RIYAMA

Mapenzi bwana! Walianza kama masihara tu huku wakiwananga vibaya walimwengu wanaofuatilia penzi lao. Mara kadhaa, Riyama Ally ambaye ni mkongwe kwenye Bongo Muvi amenukuliwa akisema umri ni namba tu hivyo hautabadilisha chochote kwenye penzi lake na msanii wa Bongo Fleva, Mystereo.

 

Kiutaniutani, kijana aliyekuwa anajitafuta, akajikuta akipata mahojiano kila pembe kutokana na penzi lake na Riyama. Kama hiyo haitoshi Riyama akauza sura kwenye video ya jamaa huo ya Usiku Mwema na nyinginezo.

 

UWOYA

Mwanamama mwenye mvuto wake Bongo Muvi, Irene Uwoya. Miaka kadhaa iliyopita aliwashangaza watu baada ya kufunga ndoa ya ghafla na msanii wa Hip Hop Bongo, Abdulaaziz Chande au Dogo Janja. Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu.

Kitendo cha Uwoya kutoka kimapenzi na Dogo Janja kinatajwa kumuongezea jamaa huyo wafuasi katika gemu na sasa ana mashabiki wengi ambao wanafuatilia na kumpa sapoti.

 

WOLPER

Hakuna ubishi kwamba miongoni mwa penzi lililovuma na kukonga nyoyo za wengi miaka kadhaa iliyopita ni lile la staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper na Konde Boy Mjeshi, Rajab Abdul au Harmonize.

 

Bila unafki, licha ya kwamba tayari Harmonize au Harmo alikuwa akijulikana, lakini mwanamama Wolper kwa kiasi chake alichangia kubusti muziki wa jamaa huyo hadi wakafikia hatua ya kuachia Ngoma ya Niambie ambayo ndani yake Wolper ndiye alikuwa video vixen.

 

ROSE NDAUKA

Miaka kadhaa iliyopita, staa mwingine wa Bongo Muvi, Rose Ndauka ilisemekana yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo. Stori hizo zilichangia kwa ukubwa Timbulo kuendelea kujulikana zaidi kimuziki.

 

SNURA

Mwanamama mwenye kiuno kama feni Bongo, Snura Mushi hakubaki nyuma kwani miaka michache iliyopita naye aliingia kwenye tetesi za kutoka kimapenzi na kijana aliyejulikana kwa jina la Minhal au Minu Calipto ambaye ni mdogo kwake kiumri.

 

Lakini hadi sasa bado wapo pamoja na tayari wamejaaliwa mtoto mmoja huku mwanamama Snura akiendelea kutoa sapoti ya kutosha kwa kijana huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva.

 

SHILOLE

Mwaka 2016, mwanamama asiyeishiwa vituko Bongo, Zuwena Mohammed au Shilole aliingia kwenye penzi zito na kijana mdogo, Naftal Mlawa almaarufu Nuh Mziwanda ambaye kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuusukuma muziki wake ambapo hadi sasa anajulikana na kupendwa na mashabiki.

 

AUNT EZEKIEL

Penzi ambalo linashika kasi kwa sasa ni la mwanamama mwenye mvuto asilia kunako Bongo Muvi, Aunt Ezekiel na msanii wa Bongo Fleva, Salmin Issah au Kusah.

Awali Kusah alikuwa anabanjuka kimapenzi na mwanamama Hellen George au Ruby hadi wakafikia hatua ya kuzaa mtoto wa kike, lakini baadaye penzi lao liliingia doa kisha wawili hao kutengana.

 

Baada ya hapo Kusah alihamishia majeshi kwa Aunt Ezekiel na nyota yake kimuziki ndiyo imezidi kukua kwani kwa sasa tayari ameshaachia ngoma yake mpya ya I Wish ambapo ndani yake mwanamama huyo ameuza nyago kama video vixen.

Stori: Memorise Richard, Bongo

Leave A Reply