Walimu Wadai Hawako Salama na Corona

SHULE  zimeshindwa kufunguliwa leo nchini Malawi baada ya walimu kugoma wakisema hawako salama katika mazingira ya kazi. Wametoa madai kadhaa kwa serikali ikiwa ni pamoja na posho ya hatari ya #COVID19.

 

 

Wiki tano zilizopita, Rais Lazarus Chakwera aliagiza shule zifungwe kutokana na ongezeko la visa na vifo vya ugonjwa huo. na zilitakiwa kufunguliwa leo baada ya maambukizi kupungua.

 

Chama cha Walimu cha Malawi (TUM) kinataka watumishi hao wapewe vifaa vya kujikinga (PPE) pamoja na mafunzo ya jinsi ya kushughulikia kesi za corona ndani ya shule zao.





Toa comment