The House of Favourite Newspapers

Waliofanya Vizuri Katika Mitihani Rorya Wapewa Zawadi, Waliofeli Wapewa Ngao

0

 

MKUU wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka ameongoza hafla ya utoaji wa zawadi ikiwemo fedha taslimu, daftari, kalamu, tuzo na ngao kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2022.

Hatua hiyo ni sehemu ya kutambua mchango na kazi kubwa waliyoifanya katika kuiinua sekta ya elimu wilayani Rorya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chikoka amesema kutolewa kwa zawadi hizo ni utaratibu ulioanzishwa kama motisha Ili kuhamasisha wanafunzi na walimu kuongeza juhudi za kufundisha na kusoma Kwa bidii na kuongeza ufaulu.

Chikoka ameongeza pia kuwa wameanzisha utoaji wa ngao ya changamoto kwa shule itakayofanya vibaya lengo ikiwa ni kuamsha ari kwa uongozi wa shule kuongeza juhudi ya kufundisha na kufanya vizuri kama ilivyo kwa shule nyingine.

Leave A Reply