The House of Favourite Newspapers

Waliomchafua Sanchi Watakufa

0

BAADA ya picha zake chafu kuzagaa mitandaoni, mrembo ambaye ni mwanamitindo ndani na nje ya nchi, Jane Rimoy ‘Sanchi’, ameibuka na kueleza kuwa waliosambaza watakufa kinywa wazi.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Sanchi alisema kuna mtu alimchezea mchezo mchafu lakini alifikiri angemuaibisha milele bila kujua Mungu yupo na anajua ukweli wa kila kitu na ndiyo maana picha moja ilijionyesha dhahiri kuwa siyo yeye.

 

“Waliofanya ule uchafu ili kuniharibia na kunichafu bila sababu za msingi wanajijua, naona kabisa watakufa kinywa wazi na wala wasifikiri wamenikomesha hapana bado nadunda kama kawaida,” alisema Sanchi.

STORI: IMELDA MTEMA

Leave A Reply