The House of Favourite Newspapers

Chambeshi Rasmi Simba, Avunja Mkataba Nkana, Kutua Dar leo

0

 

KOCHA mpya wa Simba, Mzambia, Beston Chambeshi ‘Quick Silver’, anatarajia kuingia kati ya leo Jumatatu au kesho Jumanne kwa ajili ya kusaini mkataba na timu lakini habari mpya jana alivunja mkataba wake katika klabu yake ya Nkana.

 

Chambeshi ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Mbelgiji, Patrick Aussems, anasifika kwa falsafa yake ya soka zuri, pasi na nguvu hali iliyopelekea kuwepo nafasi kubwa kulamba dili hilo.

 

Kocha huyo alitua nchini Jumatano ya wiki iliyopita kimyakimya kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mwisho kukamilisha mipango ya kukinoa kikosi hicho kilichobeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo.

 

Taarifa za uhakika ni kuwa jana Jumapili, kocha huyo aliaga rasmi kwenye klabu yake ya Nkana tayari kwa kuanza safari ya kuja nchini kujiunga na Simba ambapo anatarajia kutangazwa keshokutwa Jumatano.

 

Championi lilimtafuta kocha huyo na kutaka kujua ukweli kama ameondoka Nkana lakini hakutaka kuweza wazi zaidi ya kusema kuwa anajianda kuja nchini.

 

Championi halikuishia hapo lilifanikiwa kumnasa mtoto wake, Junior Chambeshi ambaye alisema kuwa: “Baba leo amevunja mkabata wake na Nkana kwa makubaliano ya pande zote mbili na anaondoka akiwa amewaaga Nkana vizuri lakini hajanieleza wapi anaelekea.”

Leave A Reply