The House of Favourite Newspapers

Waliotumuliwa Chadema Wapewa Rungu Kamati za Bunge

0

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, jana Januari 18 amefanya utuezi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge 17, huku pia wenyeviti wa kamati hizo wakitajwa, wakiwemo baadhi ya wabunge waliofukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 

 

Miongoni mwa wabunge waliotajwa ni Naghenjwa Kaboyoka aliyetetea uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Grace Tendega aliyeshinda uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

 

 

Naghenjwa na Tendega ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema waliofukuzwa uanachama Novemba 27, baada ya kwenda bungeni Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama. Hata hivyo, wabunge hao walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho, wakisubiri kusikilizwa.

 

 

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati hizo zinapaswa kuongozwa na wabunge wa upinzani. Mbali na Kaboyoka, kamati ya PAC imepata makamu mwenyekiti mpya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM), Japhet Hasunga.

 

 

Kwa upande wa LAAC, mbali na Tendega, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akichaguliwa Seleman Zedi Mbunge wa Bukene (CCM). Mbunge mwingine aliyetetea nafasi yake ni wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso anayeendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi kingine.

 

 

Nafasi ya umakamu imeenda kwa Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela. Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria huku nafasi ya umakamu akifanikiwa kuitetea Najma Giga.

 

 

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa amechaguliwa Mbunge wa Kuteuliwa Humphrey Polepole ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Nafasi ya umakamu mwenyekiti imekwenda kwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abdallah Chaurembo.

 

 

Mwingine aliyefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti ni Mbunge wa Mkinga (CCM) Danstan Kitandula ambaye amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini. Katika uchaguzi huo, Seifa Gulamali alichaguliwa kuwa Manonga (CCM) amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

 

 

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Christine Ishengoma amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji huku nafasi ya umakamu ikienda kwa Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM) Athuman Maige.

 

 

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) amechaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Grace Tendega huku Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Fatma Toufiq amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi huku makamu akichaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Alice Kaijage.

 

 

Kamati ya Bunge ya bajeti wamemchagua Mbunge wa Babati Vijijini (CCM) Sillo Baran huku makamu mwenyekiti akichaguliwa Mbunge wa Kilindi (CCM) Omar Kigua.

 

 

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Emmanuel Mwakasaka amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa mara nyingine huku aliyekuwa Naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Ulemavu Stella Ikupa akichaguliwa kuwa makamu.

 

 

Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma amechaguliwa Atupele Mwakibete mbunge wa Busokelo (CCM) huku umakamu mwenyekiti ukienda kwa George Malima ambaye ni Mbunge wa Mpwapwa (CCM).

 

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii amechaguliwa Dk Alyoce Kwezi (Kaliua-CCM) huku makamu wake akichaguliwa Dk Pius Chaya (Manyoni Mashariki-CCM).

 

 

Mussa Azan Zungu (Ilala-CCM) aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kipindi kilichopita amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama. Katika uchaguzi huo, wajumbe walimchagua Vincent Mbogo (Nkasi Kusini-CCM) kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika juzi.

 

 

Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira huku nafasi makamu mwenyekiti ikibakia wazi baada ya wajumbe kutofanya uchaguzi.

 

Spika Ndugai Aanika Kamati za Bunge by Eddy Nevo on Scribd

 

Leave A Reply