Wambura Ataka Wasanii Kurasimisha Kazi Zao

naibu-waziri-wa-wizara-ya-habari-utamaduni-sanaa-na-michezoNaibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, akizungumza mbele ya wanahabari.

rais-wa-taasisi-ya-tanzania-christian-deliberation-bureauRais wa Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Bureau (TCDB), Calorus Bujimu, akizungumza kwenye hafla hiyo.

wanahabari-wakichukua-matukioWanahabari wakichukua matukio.

NAIBU Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura,  amewataka wasanii nchini kurasimisha kazi zao ili kutambulika, kupata haki zao za msingi na kuongeza pato la taifa.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu wanavyotakiwa kuwa wabunifu kutokana na  vipaji walivyonavyo na namna ya kuviendeleza.

Akifafanua, Wambura alisema sanaa  ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana inayowapa fursa ya kujikwamua kiuchumi na hata kukuza pato la taifa japokuwa kuna changamoto kwa wasanii kutojitokeza au kujisajili katika sekta zinazohusika katika mambo ya hakimiliki.

Aidha alisema ili kutekeleza agizo la rais alilolitoa bungeni  kuhusu haki za wasanii, aliwataka wadau mbalimbali wa sanaa na sekta binafsi kushirikiana na serikali  kuhakikisha maslahi ya wasanii yanaboreshwa na kupiga vita uharamia.

Alichukua fursa hiyo kuwataka wasanii kufuata sheria, kanuni na taratibu kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika na masuala ya sanaa zikiwemo Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ya Bagamoyo (Tasuba), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Chama cha Hakimiliki Tanzania  (Cosota) na  Bodi ya Filamu nchini ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.

Wakati huohuo, Rais wa Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Bureau (TCDB), Calorus Bujimu, alisema taasisi yake imeandaa mpango mkakati wa kazi za wasanii nchini kwa lengo la kuibua vipaji vya wasanii chipukizi na wanaokua.

Alisema mkakati huo ni matokeo ya utafiti uliobainisha  uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji katika nyanja mbalimbali za sanaa na wanaokabiliwa na  changamoto za kiuchumi.

Na Denis Mtima/GPL.

Irene Uwoya Afanya Kufuru Birthday Yake, Amkumbuka Samwel Sitta Aliyezaliwa Naye Des. 29

Toa comment