The House of Favourite Newspapers

Wametikisa na Shepu za Kuvunja Chaga

0

FEBRUARI 2019, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Magharibi visiwani Zanzibar, ACP Hassan Nassir alipiga marufuku wanaume kukohoa au kupiga kelele wakati mwanamke mwenye makalio makubwa akikatiza mbele yao.

 

Marufuku hiyo ni kama iliwaamsha warembo waliojaaliwa shepu za kuvunja chaga kwani walicharuka vilivyo na kuanza kutupia vipande vya video kwenye mitandao ya kijamii, wakitikisa ‘mizigo’ kiasi cha kusababisha mfadhaiko kwa baadhi ya wanaume wanaovutiwa nao.

 

Mwaka 2019, baadhi ya warembo kwenye mitandao ya kijamii (socialite) walijipatia na wengine kujiongezea umaarufu kwa sababu tu ya kuwa na makalio makubwa.

 

Ukiachilia mbali kupata ustaa, lakini walijikuta wakilamba madili mbalimbali ya matangazo na ujasiriamali.

Wafuatao ni baadhi ya warembo ‘walio-trendi’ mitandaoni mwaka huu kutokana na kuwa na maumbo hayo ambayo wengine wanadaiwa kuyatengeneza;

 

JACQUELINE OBEID ‘POSHY QUEEN’

Poshy alianza kusikika alipokuwa akisoma Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilichopo Posta jijini Dar.

Poshy alikuwa akiwashangaza wanachuo wenzake kutokana na umbo lake la namba nane na kiuno cha nyigu. Siyo wanachuo pekee waliokuwa wakimmezea mate kutokana na shepu yake hiyo, bali hata madereva walikuwa wakisababisha foleni wakati wakimtazama akikatiza barabara za Posta.

 

Umbo hilo limempa Poshy umaarufu kiasi cha kuweza kujiajiri kwa kuanzisha biashara ya nguo za ndani za wanawake katika maduka yake ya Poshy Secret.

Hadi sasa, Poshy anatajwa kuwa miongoni wa warembo wenye maisha mazuri kutokana na umbo lake.

 

JANE RIMOY ‘SANCHI’

Kwa mara ya kwanza, Sanchi alionekana na Mshindi wa Big Brother Africa 2014 ambaye pia ni komediani maarufu Bongo, Idris Sultan ikidaiwa ni mpenzi wake.

Kuna waliodai kuwa Sanchi alikuja kumpindua mwigizaji Wema Isaac Sepetu aliyekuwa mpenzi wa Idris na pia kusifika kuwa na kalio kubwa ambalo sasa hivi limepungua!

 

Baada ya muda, Sanchi alianza kusifika kwa kutupia picha na video za utupu zikionesha umbo lake matata. Jambo hilo lilimfanya kuwa maarufu na kupata tenda mbalimbali za ‘kuhosti’ pati za matajiri ndani na nje ya Bongo. Mbali na hilo pia analamba madili ya matangazo ya nguo za ndani akitarajia kuzindua maduka yake ya nguo za ndani yaitwayo Sanchiworld Seductive.

 

VERA SIDIKA MUNG’ASIA

Vera ni miongoni mwa warembo maarufu zaidi nchini Kenya na Afrika Mashariki kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake matata.

 

Alianza kujulikana kama video vixien (muuza sura kwenye video za muziki) na mwanamitindo. Baadaye alijiingiza kwenye ujasiriamali wa kutangaza bidhaa mbalimbali mitandaoni. Lakini kilichompa umaarufu zaidi ni kitendo cha kuanika picha na video za kalio lake kubwa na sasa ni mmoja wa warembo tishio kwenye mitandao ya kijamii.

 

Alitingisha vilivyo mwaka huu alipotinga kwenye baby shower ya mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna akiwa amevaa nguo inayoonesha ‘kufuli’ na kalio lake laivu bila chenga.

MWANAHERI AHMED ‘MWANA’

Huyu ni mwigizaji wa Bongo Movies anayekimbiza kwenye Tamthiliya ya Kapuni akitumia jina la Joyce.

Pamoja na uigizaji, umaarufu mkubwa ameupata kutokana na umbo lake kwenye mitandao ya kijamii.

Pamoja na kwamba, huwa haweki picha za utupu, lakini hata akitupia picha za heshima, huwa anakuwa gumzo kutokana na umbo lake.

 

   SKYNER ALLY ‘SKAINA’

Skaina alikuwa mmoja wa waigizaji bora wa Bongo Movies kabla ya kuacha kuigiza. Ni miongoni mwa waigizaji wenye maumbo ya kutetemesha ambapo kwa sasa amegeukia matangazo ya nguo na ujasiriamali baada ya jina lake kuwa kubwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na umbo lake.

 

 

SASHA KASSIM

Sasha alianza kujulikana kama video vixen kisha mwanamitindo na mwigizaji wa Bongo Movies. Kilichompaisha Sasha ni umbo lake matata ambapo amekuwa akitupia picha na video akitingisha sehemu za nyuma kiasi cha wanaume kujirushia kwenye makundi ya WhatsApp.

 

Pamoja na kwamba ni mwanachuo wa Chuo cha Udaktari cha Bugando jijini Mwanza, lakini umbo lake limempa umaarufu mitandaoni kiasi cha kuanzisha biashara yake ya mavazi akitumia jina la Sasha Kassim FashionTZ.

Makala: Imelda Mtema

Leave A Reply