The House of Favourite Newspapers

Wamarekani Kuamua Leo, Trump Au Biden

0

 

RAIS wa Marekani, Donald Trump, na mshindani wake, Joe Biden, wamemaliza kampeni zao kwenye ngome zao muhimu huku kila mmoja akinadi sera zake kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika leo Novemba 3  utakaochagua viongozi watakaoongoza kwa miaka minne ijayo.

 

Biden alifanya kampeni Pennsylvania na Ohio, wakati  Trump akiwa Winsconsin, Michigan, North Carolina na Pennsylvania.

 

Wagombea hao wawili watachuana vikali kuwania kiti cha urais wakati taifa hilo limekaa njia panda kutokana na serikali ya Trump ilivyopambana na janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.

 

Kura za awali zinaonyesha   Wamarekani zaidi ya milioni 93 wameshapiga kura na kila upande unaonyesha  dalili kuwa utaibuka na ushindi.

 

Hata hivyo, mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden, anaelekea kuwa na uwezekano zaidi ya kuwapata wajumbe 270 wa kumpigia kura na kuibuka kidedea kwenye uchaguzi huo.

 

Wakati Wamarekani wakijitayarisha kupiga kura leo hii, watu zaidi ya laki mbili (200,000)  wameshakufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19, hivyo kumweka Trump kwenye wakati mgumu wa kutetea kiti chake kuelekea kwenye uchaguzi huo.

Leave A Reply