Telesphory ambaye ni shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo aliyaeleza hayo jana Alhamisi Julai 11, 2019 mbele ya hakimu mkazi, Catherine Kihoja na wakili wa Serikali, Grace Lwila katika kesi ya jinai namba 65 ya mwaka 2016.
Akitoa ushahidi katika kesi hiyo, Telesphory alieleza kuwa majukumu yake ni kufanya doria mitandaoni na kuchambua data za kielektroniki.
Amedai kuwa Juni 13, 2016 akiwa ofisini kwake alipewa maelekezo na Inspekta Beatrice kwenda katika chuo hicho kuna mshtakiwa ametuma picha ya rais akiwa amevaa Hijab katika kundi la mtandao wa kijamii la WhatsApp la Human Resource Menagement.
“Tulikwenda hadi chuoni hapo tutaonana na mlezi wa mwanafunzi, Herma Frank, tukamueleza tunawahitaji wanafunzi hao na alikiri kuwa wapo akatuitia,” amesema shahidi huyo.
Amesema wanafunzi hao waliitwa na alifanya mahojiano na Amenitha aliyekiri kuifahamu picha hiyo na kwamba aliituma katika kundi hilo.
Amebainisha kuwa mwanafunzi huyo alipoulizwa alikoipata, alieleza kuwa ilitumwa katika kundi la mtandao huo la Empire na rafiki yake, Mariam.
Alisema pia walimhoji Agnes aliyekiri kuitambua picha hiyo na kueleza kuwa ilitumwa katika kundi la St Mary’s Ulete lakini alishindwa kukumbuka nani aliituma.
Walisambaza katika mitandao ya kijamii ya WhatsApp picha hizo zikimuonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa vazi hilo linalovaliwa na wanawake wa dini ya Kiislam, jambo ambalo si kweli.
Hakimu Kihoja ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 22 na 23, 2019 na kuutaka upande wa mashtaka kupeleka mashahidi wa kutosha ili kesi imalizike mapema.
Comments are closed.