The House of Favourite Newspapers

Bigirimana, Kalengo wamvuta fasta Zahera Morogoro

UWEPO wa mastaa wapya wa Yanga kambini mkoani Morogoro wakiwemo Issa Bigirimana na Maybin Kalengo, umefanya kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera fasta arudi nchini kwa ajili ya kuungana nao.

 

Yanga wameanza kambi yako katika Chuo cha Biblia, Bigwa mkoani Morogoro ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

 

Kambi hiyo imekusanya wachezaji wote wakiwemo wale wapya ambao wamesajiliwa, baadhi yao ni Kalengo, Bigirimana, Patrick Sibomana, Abdulaziz Makame, Juma Balinya na wengineo ambapo kwa sasa kambi hiyo inasimamiwa na kocha msaidizi, Noel Mwandila.

Zahera amekosekana katika kikosi hicho kutokana na sasa kuwepo barani Ulaya akiwa mapumzikoni baada ya kutoka katika majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo ambayo iling’olewa na Madagascar katika hatua ya 16 bora kwenye Afcon.

 

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Championi Ijumaa, kuwa muda wowote wiki ijayo kocha huyo ataungana na wachezaji hao kwa ajili ya kuendelea na kambi hiyo ambayo ina ulinzi wa hatari.

 

“Kocha yupo mapumzikoni kidogo baada ya kutoka Afcon na timu yake ya taifa, lakini kuanzia wiki ijayo basi atarejea fasta kuungana kuendelea na kambi,” alisema Hafidh.

Said Ally, Dar es Salaam

NOMA! MIKAKATI Ya YANGA Hii Ni BALAA, Dismas Ten Aelezea..!

Comments are closed.