WANACHUO WALIOTENGENEZA MITA YA MAJI WATUA GLOBAL
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha St. Joseph cha jijini Dar es Salaam waliobuni mita ya kisasa na mfumo wa kulipia bili ya maji inayofanya kazi kwa mfumo kama wa LUKU na inatumia umeme wa jua, Ijumaa, Julai 19, 2019, wamefanya ziara ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar wakiambatana na mwalimu wao kuonyesha uvumbuzi wao ambao unaenda kutatua changamoto za malipo ya huduma ya maji nchini.
Mita hiyo imetengenezwa na Khadija Mustapha, Edina Pesha na Hashim Shukuru kwa muda wa wa miezi minane na wametumia kiasi cha Tsh. 900,000/- kwa kununua baadhi ya vifaa kama mabomba ya maji, Micro controller, Solar Panel, Valve, mbao, n.k
Wakiongea na +255 Global Radio wamesema wanaendelea kuboresha mfumo huo ili kuwasadia watumiaji wa maji nchini na wanatarajia wateja wao kuwa taasisi za serikali na watu binafsi.
Kwa mujibu wa wanachuo hao, mteja atakayatumia mita hiyo atakuwa akilipia bili kupitia simu yake ya mkononi na hakuna mteja atakayeweza kutumia maji bila kulipia na kwamba wateja wakaojaribu kuwaibia kupitia mita hiyo watatumiwa ujkumbe maalum wa kuwajulisha mita namba ambayo inataka kufanya uhalifu huo.
Pamoja na uvumbuzi huo, wanatarajia kutafuta mfadhili wa kuwawezesha kutengeneza mita hizo na kuzisambaza kwenye jamii na kufungua kiwanda kwa ajili ya kubuni vitu mbalimbali vitakavyowawezeha Watanzania kutatua changamoto zao.
PICHA NA GLOBAL RADIO
Comments are closed.