WANAFUNZI kutoka Chuo Kikuu cha Case Western Reserve University cha Marekani mapema leo wamepata fursa ya kutembelea makao makuu ya ofisi za Global Group na kujionea namna kampuni hiyo inavyojiendesha katika shughuli zake mbalimbali za kihabari.
Ugeni huo ulioambatana na kiongozi wao, Michael Goldberg ambaye ni mhadhiri katika chuo hicho, umepokelewa na Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho na Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Salehe Ally, ambapo kwa pamoja waliwatembeza katika ofisi zote zilizopo katika jengo hilo na kupata fursa ya kuwaeleza mambo machache ya kiutendaji.
Lengo la ziara yao, ni kutaka kujua jinsi wajasiriamali wa Tanzania wanavyofanya shughuli zao, changamoto wanazokumbana nazo na pia kutoa misaada kwa wale wenye biashara endelevu, zinazosaidia kutatua changamoto za jamii inayowazunguka.
PICHA: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL
Comments are closed.