The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Waomba Serikali Kupata Miti ya Matunda Mashuleni

0
Wanafunzi wa shule ya msingi Matwiga iliyokoa Kata ya Misheni wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wameiomba Serikali ielekeze nguvu kupanda miti ya matunda mashuleni ili iwasaidie kupata lishe bora.
Ombi hilo limetolewa leo marchi 21,2024 mwaka  huu  na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kwenye maadhimisho  ya Misitu duniani ambapo wilayani Sengerema yameadhimishwa kwa upande miti 1000 kwenye ya msingi Matwiga.
Habiba Bakari  ni mwanafunzi wa shule ya msingi Matwiga anayesoma darasa sita amesema licha ya Serikali kuelekeza  nguvu kupanda miti ya mbao na kivuli mashuleni pia ielekeze nguvu kupanda miti ya matunda mashuleni.
Ameomba miti ya matunda aina ya maembe, Parachichi, machungwa , machenza na mapera nayo ipandwe mashule ili iwasaidie wanafunzi kupata lishe wanapokuwa shuleni.
Huku Martha Charles mwanafunzi wa darasa la sita shuleni hapo ameiomba Serikali kuweka nguvu katika suala ya uhifadhi wa mazingira Ili kuokoa nchi kuwa jangwa na kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.
” Watu wamekuwa wakikata miti ovyo na kusababisha uharibifu wa mazingira hivyo ameiomba Serikali iweke nguvu za kuwadhibiti kukomesha uharibifu huo, amesema Charles.
Mhifadhi Misitu Wilaya ya Sengerema  kutoa wakala ya misitu Tanzania (TFS) James Aloyce amesema lengo la Serikali kila mwaka ni kupanda miti hivyo  wanaotesha miti zaidi ya 200,000 kwa mwaka kwa ajili ya kugawa kwenye taasisi mbalimbali ili ipandwe na kutunza mazingira.
Katika maadhimisho ya msitu duniani yaliyofanyika wilayani Sengerema TFS  wamepanda 1000 aina ya kalitusi kwenye shule ya msingi Matwiga lengo nikutunza mazingira kwenye shule hiyo.
“Miti hii inatolewa bure kwenye kitaru chetu hivyo wananchi na taasisi za Serikali na watu binafsi wajitokeze kuchukuwa miti wakapande kutunza mazingira,amesema Aloyce.
Cuthbert Mdala ni Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema amembaye amemwakilisha mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Nganga kwenye maadhisho hayo ameelekeza miti hiyo iliyopandwa itunze ili kuhifadhi mazingira.
Suala la uhifadhi wa mazingira ni letu  hivyo tunapaswa kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuacha kukata miti ovyo.
Kwa upande wake mwalimu mkuu shule ya msingi Matwiga amewashukuru wakala wa misitu Tanzania (TFS) kutoa Miche ya miti 1000 kwa ajili ya kupanda kwenye shule hiyo ili kuhifadhi mazingira.
Tandi Laizer ni ofisa mazingira Halmashauri ya Sengerema ameseme mikakati waliyonayo ya utunzaji mazingira ni kuelimisha jamii juu kutunza mazingira kwa kupanda miti,kuboresha utunzaji mazingira kwa kuhimiza wananchi kushiriki kila jumamos ya kwanza ya mwezi Kushiriki kupanda miti na kuhifadhi mazingira
Wakala ya misitu Tanzania TFS wameendelea na kampeni ya utoaji na upandaji miti kwenye taasisi za Serikali ili kuitunza mazingira ambapo kwenye maadhisho ya misitu dunia wamepanda miti 1000 kwenye shule ya msingi Matwiga ili kuhifadhi mazingira.
Leave A Reply