The House of Favourite Newspapers

Mpango Aimwagia Sifa Wizara Ya Maji, Aisifu Kwa Chenji Kubaki

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji wa Kikafu – Bomang’ombe uliopo katika Kijiji cha Kwasadala Wilaya ya Hai akiwa ziarani Mkoani Kilimanjaro tarehe 20 Machi 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ameipongeza Wizara ya Maji kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maji nchini.

Ametoa pongezi hizo Machi 20, 2024 wakati akizindua mradi wa maji wa Kikafu-Bomang’ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro uliojengwa kwa ustadi mzuri huku chenji ya zaidi ya milioni 577.6 zikiwa zibaki baada ya utekelezaji.

Aidha Mhe. Mpango amewapongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutekeleza mradi na kubakisha fedha na kuwaagiza fedha hizo zilibaki kwenye mradi huo zitumike kupeleka maji kwa wananchi wa eneo la Matowo Wilayani Hai.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifungulia maji mara baada ya kuzindua Mradi wa Maji wa Kikafu – Bomang’ombe uliopo katika Kijiji cha Kwasadala Wilaya ya Hai akiwa ziarani Mkoani Kilimanjaro tarehe 20 Machi 2024.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi, Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafiwa Mazingira Vijijini Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Weransari Munisi amesema gharama za mradi huo kwa mjibu wa mkataba ilikuwa utekelezwe kwa shilingi 3,392,463,389.08, kutokana na usimamizi mzuri mradi huo umekamilika kwa gharama ya shilingi 2,814,854,757.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemhakikishia Mhe. Makamu wa Rais kwamba Wizara ya Maji itaendelea na jitihada za kuhakikisha inasimamia maagizo ili kuhakikisha kila kona ya nchi inafikiwa na huduma ya maji.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akivuta kitambaa kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Kikafu – Bomang’ombe uliopo katika Kijiji cha Kwasadala Wilaya ya Hai akiwa ziarani Mkoani Kilimanjaro tarehe 20 Machi 2024.

Amesema yako mafanikio ambayo wizara imeyapata ndani ya nje ya nchi ikiwemo kuwa ya kwanza katika utekelezaji wa miradi ya maji Duniani kupitia mradi wa Lipa kwa Matokeo (PforR) kwa miaka miwili mfululizo na kwamba mafanikio hayo watayaendeleza.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwasalimu viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika eneo la Kwasadala Wilaya ya Hai kwaajili ya kuzindua Mradi wa Maji wa Kikafu – Bomang’ombe akiwa ziarani Mkoani Kilimanjaro tarehe 20 Machi 2024.

Leave A Reply