The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Wafariki Katika Mlipuko wa Lori la Mafuta

0

WATU wapatao 25 wamefariki nchini Nigeria baada ya lori kumshinda dereva  na kukosa uelekeo kisha kugonga magari mengine na tenki lake la mafuta ya petroli kulipuka katika katika eneo la Kogi, mjini Lokoja.

 

Msemaji wa polisi mjini Lokoja, Willy Aya, amesema kuwa baadhi ya watu, wakiwemo wanafunzi wa shule, waliungua vibaya na hawawezi kutambulika.

 

Ajali za mlipuko wa malori ya mafuta nchini Nigeria zimekuwa nyingi. Mwezi Juni, watu wanne waliukufa mjini Lagos baada ya mlipuko wa magari manne. Wiki iliyopita tenki lingine la mafuta ya petroli lilipuka.

 

Leave A Reply