The House of Favourite Newspapers

Wanahabari Wanolewa Kuhusu Usiri Wa Taarifa Mtandaoni

0
Rais wa shirika la Internet Society Tanzania, Nazarius Kirama.

Dar es Salaam 20, Desemba 2023: Shirika la Huduma za Mtandao kwa Jamii, Internet Society limewanoa wanahabari na kuwapa wanahabari elimu ya ulinzi wa taarifa mtandaoni.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Rais wa shirika hilo hapa nchini, Nazarius Kirama alisema kuna umuhimu mkubwa sana katika suala la ulinzi mtandaoni kati ya mtu na mtu, taasisi na taasisi au vinginevyo.

Sehemu ya Wanahabari kwenye mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yalifanyika Ukumbi wa Old Boma, Posta jijini Dar na kuhudhuriwa na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.

Akihitimisha mafunzo hayo Nazarius aliwasisitiza kuyatumia mafunzo hayo katika kuielimisha jamii kwakuwa wao ndiyo wenye nguvu kubwa katika kufikisha taarifa kwa jamii.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply