The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 8 wa UN Wajeruhiwa Katika Mlipuko wa Bomu Katika eneo la Mali la Timbuktu

0

Wanajeshi walinda amani wanane wa Umoja wa mataifa wamejeruhiwa Alhamisi katika mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini katika eneo la Mali la Timbuktu linalokumbwa na uasi wa wanamgambo wa kiislamu, Umoja wa mataifa umesema.

 

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni wanajeshi wa Burkina Faso wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa(MINUSMA), afisa wa Umoja wa mataifa ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia AFP.

 

Msemaji wa MINUSMA Olivier Salgado amesema kwenye Twitter kwamba shambulio hilo lilitokea karibu na mji wa Ber, katika eneo la Timbuktu.

 

Walinda amani wanne wa Umoja wa mataifa waliuawa mwezi huu katika mashambulizi yaliyofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu kaskazini na katikati mwa Mali.

 

Kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani nchini Mali (MINUSMA) chenye wanajeshi 13,000, ni moja ya vikosi vikubwa vya Umoja wa mataifa, na huendesha operesheni zake katika eneo la hatari.

 

MINUSMA inasema wanajeshi wake 175 walifariki katika mashambulizi.

Mazungumzo yanaendelea ili kuongeza muhula wa kikosi hicho cha Umoja wa mataifa nchini Mali.

DRONE VIDEO: RAIS SAMIA ALIVYOWAKOSHA WAKULIMA WA KOROSHO MTWARA, SASA FULL SHANGWE..

Leave A Reply