The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi Urusi Waishiwa Mahitaji Muhimu

0

KAMPUNI ya kijasusi ya ShadowBreak ya nchini Uingereza, imedai kwamba imenasa mawasiliano kati ya wanajeshi wa Urusi waliopo uwanja wa vita wakiwasiliana na viongozi wao ambapo majibizano yao, yanaonesha kwamba wanajeshi hao hawana tena morali ya kuendelea kupigana na wameishiwa mahitaji muhimu ikiwemo chakula.

Kampuni hiyo imedai kwamba imenasa sauti za wanajeshi wa Urusi, wakifokeana, kutukanana na kulalamikiana wao kwa wao, ambapo mwanajeshi mmoja amesikika akilia katika majibizano hayo na viongozi wao.

Gazeti la The Telegraph, limedai kuwa limesikiliza sauti hizo za mawasiliano hayo yaliyovujishwa na Kampuni ya ShadowBreak ambapo mwanajeshi mmoja amesikika akipandisha jazba akihoji kwa nini viongozi wao hawawafikishii mahitaji muhimu ikiwemo chakula?

Mwanzilishi wa Kampuni ya Ujasusi ya ShadowBreak, Samuel Cardillo ameliambia Gazeti la The Telegraph kwamba vijana wake wamefanikiwa kuyanasa mazungumzo hayo kupitia antena maalum za kuingilia mawasiliano.

“Tulichokibaini ni kwamba hakuna maelewano kwa upande wa mawasiliano ya Jeshi la Urusi. Hawajui ni nini kinachoendelea na nini itakuwa hatma yao na hawajui namna ya kuwasiliana vizuri,” amenukuliwa Cardillo.

Leave A Reply