The House of Favourite Newspapers

Nabi Ataja Kinachomnyima Mabao Makambo Yanga

0

KWA mara ya kwanza Kocha Mkuu waYanga, Mtunisia Nasreddine Nabi ameibuka na kutaja sababu inayomfanya mshambuliaje wake Heritier Makambo kushindwa kufunga mabao.

 

Nyota huyo ameonekana kutokuwa na msimu mzuri kwake kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Tangu kuanza kwa msimu huu mshambuliaji
huyo hajafanikiwa kufunga bao katika ligi huku akipata ugumu wa namba kutoka kwa Mkongomani mwenzake, Fiston Mayele aliyekuwepo katika ubora mkubwa.


Akizungumza na Championi Jumatano, mara
baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Nabi alisema ukame wa mabao unamfanya atoke mchezoni, apoteze umakini na kujikuta kukosa nafasi nyingi za wazi za kufunga.


Nabi alisema kuwa mshambuliaji huyo
anatakiwa kutuliza akili yake na kupunguza presha anayoipata kutoka
kwa mshambuliaji
mwenzake Mayele mwenye mabao tisa katika ligi.


Aliongeza kuwa
anaamini kama akituliza akili zake, basi atafunga idadi kubwa ya mabao kutokana na kiwango kizuri alichonacho hivi sasa ambacho anakionyesha uwanjani.


“Kisaikolojia Makambo hayupo sawa, hiyo ni
kutokana na presha kubwa anayoipata kutoka kwa mshambuliaji mwenzake Mayele aliyekuwa katika kiwango bora hivi sasa.

 

“Hiyo inaweza kumkuta mchezaji yeyote mwenzake anapofanya vizuri pale anapopata nafasi ya kucheza, Makambo anatakiwa kupunguza presha itakayomfanya acheze kwa kujiamini.

 

“Siku zote mshambuliaji unapopoteza nafasi za wazi za kufunga, hali ya kujiamini inapungua na kujikuta mchezaji akitumia vibaya nafasi ya kufunga kama ilivyokuwa kwa Makambo ambaye leo (Jumapili) tulipocheza dhidi ya Kagera alishindwa kutumia nafasi zaidi ya moja za wazi za kufunga, hiyo imetokana na presha aliyokuwa nayo
hivi sasa anatamani kufunga lakini anashindwa
kutokana na kupania,” alisema Nabi na kuongeza kuwa.
“Ninaamini atatulia na kucheza vizuri ikiwemo
kufunga mabao mara baada ya kumtengeneza kisaikolojia, kama kocha hilo ndiyo jukumu langu nitajitahidi kumbadilisha na kumuweka sawa.”

Leave A Reply