The House of Favourite Newspapers

Wananchi Mlalo: Rashid Shangazi ni chaguo sahihi kwa maendeleo ya kweli

0

Rashidi Shangazi akinadiwa kwa wananchi na mgombea urais wa CCM, John Magufuli.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu akiwa na Rashidi Shangazi.

Rashidi Shangazi akiwa katika moja ya kampeni zake.

Januari Makamba, Mwigulu Nchme na Rashidi Shangazi jimboni Mlalo.

Wananchi wa Jimbo la Mlalo lililopo Wilayani Lushoto mkono Tanga wamesema wana imani kubwa na mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rashid Shangazi wakiamini ndiye atakayeleta maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu.

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti kwenye kampeni zilizofanyika jimboni humo, wananchi hao wamesema Shangazi ni kijana wa kipekee ambaye anazijua shida wa watu wa Mlalo hivyo wanaamini wakimpa nafasi ya kuwa mbunge wao, hatawaangusha.
“Sisi kwa kweli tunamtaka Shangazi, hao wengine wanajisumbua tu. Nasema hivyo kwa sababu yeye alianza kufanya mambo ya kimaendeleo katika jimbo letu hata kabla ya kuwa na ndoto za kugombea, sasa jiulize mtu kama huyu mkimpa ubunge itakuwaje?
“Mimi naomba wana Mlalo wenzangu tumpe kura aweze kutuletea mabadiliko ya kweli, hao wengine wanatulaghai tu lakini chaguo sahihi ni Shangazi hivyo tusifanye makosa Oktoba 25,” alisema Hamisi Hoza mkazi wa Lukozi.
Naye Husna Shekigulio wa Kifulio alisema: “Unajua chema chajiuza, watu wamelalamika sana kipindi cha uongozi wa Ngwilizi (Hassan Ngwilizi, mbunge aliyepita) lakini sasa Mungu ametuletea huyu kijana, kwanza si mtu wa kupenda kukaa mjini sana, anafanya shughuli zake jijini Dar lakini mara kwa mara yuko Mlalo na amechangia sana maendeleo ya Mlalo.
“Ndiyo maana nawasihi wale ambao wana mapenzi na jimbo letu kutodanganyika na sera na wapinzani, Rashid Shangazi anatosha.”
Akizungumzia alivyojipanga katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, Shangazi alisema: “Watu wa Jimbo la Mlalo wananijua vizuri sana, sina haja ya kutoa ahadi nyingi ila nataka kuifanya Mlalo iwe ya kuigwa, nitaleta maendeleo ambayo wananchi wa jimbo hili wanayahitaji.
“Shida zao nazijua vizuri, wanipe nafasi niwatumikie na naahidi tu kwamba kila atakayenipa kura Oktoba 25, hatajuta kwani atakuwa amefanya maamuzi sahihi.”

(Habari/Picha: Amrani Kaima)

Leave A Reply