The House of Favourite Newspapers

Wananchi wa Buchosa Kulipwa Fidia Zao Kabla ya Ujenzi wa Barabara ya Lami

0
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo akitoa mchango Bungeni

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imesema kuwa Wananchi wa Jimbo la Buchosa watalipwa fidia zao kupisha ujenzi wa barabara ya Lami inayotarajiwa kujengwa kuanzia Jimbo la Sengerema kuelekea Jimbo la Buchosa, huku ikibainishwa kuwa malipo hayo yatalipwa kabla ya ujenzi huo kuanza.

 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Godfrey Kasekenya wakati akijibu swali Bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya CCM Eric Shigongo juu ya ni lini hasa wananchi wa Buchosa watalipwa fidia zao kupisha ujenzi wa Barabara hiyo.

 

Aidha katika hatua nyingine Mbunge Shigongo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ianzie ujenzi wa Barabara hiyo katika Jimbo la Buchosa kwenda Sengerema jambo ambalo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amebainisha kuwa mchakato tayari umeshaanza wa utekelezaji wa ujenzi huo hivyo mradi utaendelea kama kawaida kutoka Jimbo la Sengerema kwenda Jimbo la Buchosa kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali

 

Bunge la Tisa Mkutano wa kumi kikao cha nne limeendelea leo mkoani Dodoma ambapo wabunge wameendelea kuibana serikali kwa maswali na hoja zenye nguvu.

Leave A Reply