The House of Favourite Newspapers

Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kenya Warejesha begi lenye Milioni 44 Kwa Mtalii

0

Wafanyakazi wawili wa uwanja wa ndege wa Kenya na afisa wa polisi wamejizolea sifa baada ya kurudisha begi lililokuwa limebeba takriban $19,000 sawa na milioni 44 za Kitaanzania na vitu vingine vya thamani kwa mtalii wa Uingereza.

 

Mtalii huyo alikuwa katika kundi ambalo lilikuwa limerejea kutoka safarini katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara alipopoteza begi katika uwanja wa ndege wa Wilson katika mji mkuu, Nairobi.

 

Wafanyikazi wa uwanja wa ndege na polisi mwanamke walipata begi na kulikagua ikiwa hakuna vilipuzi kabla ya mmiliki kuarifiwa .

 

“Pesa zote – jumla ya dola 19,000 na baadhi ya maelfu ya shilingi za Kenya zote zilikuwa ziko sawa. Kadi zangu zote zilipatikana zikiwa humo ndani. Vitu vingine vyote vya thamani vilivyojumuisha mavazi niliyopewa na marehemu bibi yangu pia yalikuwa safi. Ilikuwa ndoto yangu ya mchana. ” mtalii aliyetambulika kama Benson alisema katika barua pepe ya shukrani kwa polisi wa Kenya

 

Alisema alibeba kiasi kikubwa cha fedha ili kufanikisha safari na shughuli za kikundi chake.

 

Msimamizi wa usalama wa uwanja huo wa ndege, Joseph Kabangi, aliambia runinga ya Citizen ya nchini kuwa “uadilifu ndio thamani kuu” miongoni mwa wafanyikazi katika uwanja huo.

KIKOSI cha YANGA KILIVYOWAFUATA CLUB AFRICAIN, MAYELE, KI AZIZ HATARI…

Leave A Reply