Wakati sikuku ya Krismasi ikiwa imemalizika Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo amesherehekea sikukuu hiyo kwa kufanya Misa fupi ya kuwakumbuka wapendwa wake waliotangalia mbele za haki akiwemo baba yake mzazi Marehemu, James Bukumbi na Bi. Asteria Kapela ambao wote wapo mbele za haki.
Akiendesha ibada fupi Paroko wa Kanisa Katoliki Mwangika Parokia ya Mt. Yakobo Mkuu, Padri Hilary Faraja amewataka wakazi wa Bupandwa na vitongoji vingine vilivyoungana katika misa hiyo kutenda matendo mema yenye kuumpendeza mungu katika kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Amesema kuwa mwanadamu anapaswa kufanya yale yote yanayompendeza Mungu, kuoneshaa upendo kwa ndugu jamaa na marafiki, kusaidia familia zisizojiweza kwa kutoa msaada.
Pia Paroko huyo amewataka viongozi walio katika nyadhifa mbalimbali kuenenda na nyakati ambapo kwa sasa dunia inaenda katika digitali na hivyo kutumia fursa hiyo kuonesha yale wanayoyafanya katika maeneo yao kupitia mitandao mbalimbali ili jamii iweze kuyaona.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe. Eric Shigongo amewashukuru wananchi wote waliofika kuungana na wanafamilia ya Bukumbi na kwamba wanawapenda sana na kama familia itaendelea kushirikiana katika shughuli zote za kijamii na kifamilia ili kuendeleza umoja waliouacha wazazi wao ambao siku ya leo wanakumbukwa kwa kuwaombea.