The House of Favourite Newspapers

Wananchi Waliyowazomea Watalii na Kuwaita Corona Yawakuta

0

MKUU wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Christopher Ngubiagai amekemea vikali na kuahidi kuwachulia hatua kali, baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwazomea watalii wa kizungu na kuwaita majina ya corona baada ya watalii hao kutembelea wilaya hiyo.

 

Ngubiagai ameyasema hayo alipokuwa akitoa maelekezo juu ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona ofisini kwake huku akiagiza taasisi zote binafsi na za umma wilayani humo kutengeneza sehemu ya kunawia mikono watu mbalimbali pindi waingiapo ofisi zao.

 

Ngubiagai ameongeza kwa kusema licha ya ustarabu wa wananchi wa Kilwa kusalimiana kwa kupeana mikono nivvyema kipindi hiki waepuke kusalimiana kwa kupeana mikono.

 

Mpaka sasa mataifa mataifa 180 yameathirika kutokana na virusi hivyo huku watu 246,594 wakiathirika na virus hivyo huku watu 10,050 wakipoteza maisha na 88,486 wakipona virusi hiyo.

Leave A Reply