The House of Favourite Newspapers

Wananchi Zanzibar Wafurahishwa na Elimu ya TMA

0
Matukio picha mbalimbali wakati wananchi na wageni wakiendelea kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa kutoka kwa wataalam wa hali ya hewa kwenye banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Dole.
Baadhi ya wananchi wakisaini kitabu cha wageni waliofika katika banda la TMA  kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa.
Elimu ikitolewa ndani ya Banda la TMA.
Mwananchi akiendelea kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa kutoka kwa mtaalam wa hali ya hewa kwenye banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
…Elimu ya sayansi ya hali ya hewa ikiendelea  kutolewa na mtaalam wa hali ya hewa kwenye banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Matukio picha mbalimbali wakati wananchi na wageni wakiendelea kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa kutoka kwa wataalam wa hali ya hewa kwenye banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Dole, Kizambani – Unguja.
Elimu ikiendelewa kutolewa na waalam wa TMA kwenye banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Dole, Kizambani, Unguja.
Mwanadada kutoka TMA akitoa elimu ya sayansi ya hali ya hewa kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la maonesho.
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), inashiriki katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Dole, Kizimbani – Unguja, kuanzia Tarehe 04-08 Agosti, 2020. Yenye kauli mbiu ya ” tudumishe amani na utulivu kwa maendeleo endelevu ya Taifa letu la Tanzania.”
 
Wageni mbalimbali waliotembelea banda la TMA wameonesha kufurahishwa na namna elimu ya hali ya hewa inavyotolewa bandani hapo na wengi wao wamesisitiza TMA kuendelea kubuni njia nyingine zaidi za kufikisha elimu hiyo kwa wananchi wa visiwani hapo.
 
Aidha, wataalam wa hali ya hewa toka TMA wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi, usafiri wa anga na maji n.k ili kuelewa namna ya kutumia taarifa za hali  ya hewa kwa usahihi na kuongeza uzalishaji wa malighafi kupitia sekta zao na kujiepusha na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa sambamba na kutambua njia zitumikazo na Mamlaka katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa wananchi ikiwemo mitandao ya kijamii.
Leave A Reply