The House of Favourite Newspapers

Wanasimba Mkiungana Kwa Moyo Safi, Mtafika Mbali

0
Mashabiki wa Timu ya Simba.

LEO Jumanne, Klabu ya Simba inaadhimisha miaka 81 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936 ambapo kutakuwa na kilele cha Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Simba ambayo ni klabu ya pili kwa ukongwe hapa nchini baada ya Yanga, kwa zaidi ya miaka nane imekuwa na utaratibu wa kuwa na tamasha hilo ambalo hulitumia kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kutambulisha kikosi chake cha msimu pamoja na jezi watakazozitumia.

 

Wakati wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wakijiandaa na tamasha hilo, kuna hali ya sintofahamu baina yao ambapo tayari tumesikia kuna upande umeukataa mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 13, mwaka huu.

Mbali na hivyo, pia hawataki kuona mabadiliko yakifanyika kutokana na mfanyabiashara na mfadhili wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutangaza kutaka kuwekeza klabuni hapo.

 

Championi ni wapenda maendeleo ya soka hapa nchini, tunaomba Wanasimba wote mkae chini, muelewane ili mwisho wake muwe kitu kimoja katika kuijenga klabu yenu.

Soka la sasa limebadilika na linahitaji uwekezaji mkubwa katika klabu zetu ili kupiga hatua, tumeona klabu mbalimbali duniani zikiingia ubia na mashirika au wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuziinua timu zao kiuchumi. Hivyo basi lifikirieni jambo hili kwa kina.

 

Hivi mnajua kama mpo katika siku yenu muhimu ya Simba Day? Sasa inakuwaje mnagawanyika vipande viwili wakati mlitakiwa katika sherehe kama hizi ndiyo muda muafaka wa kusahau yaliyopita na kuuanza ukurasa mpya wa maendeleo!

Shuhudia Niyonzima Alivyoanza Rasmi Mazoezi na Okwi Simba

Leave A Reply