The House of Favourite Newspapers

Wanne Mbaroni Tuhuma za Mauaji Mwanza – Video

0

POLISI Mkoa wa Mwanza inawashikilia watu wanne kwa tuhuma za makosa ya kupanga tukio la mauaji ya mtu mmoja wilayani Ukerewe.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa na Kamanda wa Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne Muliro, watu hao ni Magesa Simon Wile (50) mkazi wa Nyamagana, Makanje Mgeta (28) mkazi wa Chibasi, Mkapa Magesa Simon (24) mkazi wa Nyamagana na Selestini Datusi (22) mkazi wa Nyamaga.

 

Wanashtakiwa kwa kudaiwa kupanga mauaji ya Andrew Magai (48) mkazi wa Chibasi, usiku wa Agosti 25, 2020 kwa madai kwamba marehemu alisafirisha watu kwenda kuvunja nyumbani kwa mtu aitwaye Magesa Simon Wile.

 

Upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.

 

Leave A Reply